- UTANGULIZI:
Utume wa Legio ya Maria katika Parokia ya K/Ndege ulianzishwa mwezi Mei mwaka 1990 na jina la “Praesidium” (Kikundi cha Utume) lililochaguliwa ni “Malkia wa Rosari Takatifu”. Utaratibu wa majina kwa kila Praesidium hutokana na sifa za / Litania ya Mama Bikira Maria.
Wanachama wa kwanza wa Praesidium waliweka Ahadi tarehe 23/10/1990. Hadi sasa Utume huu una wanachama wapatao 32 na Uongozi ni kama ifuatavyo:-
- Mwenyekiti – Carlos Kidiru
- Makamu Mwenyekiti – Maria Mahelela
- Katibu – Elizabeth Joseph
- Mhazini – Annamaria Kalani

- LENGO LA UTUME:
Lengo Kuu la Utume wa Legio ya Maria ni:
Kwanza, Utakatifu binafsi kwa mwanachama na halafu kuwasaidia wengine kuondokana na dhambi ili kuupata utakatifu na hatimaye wote tufikie kwa Baba Mbinguni kupitia Maombezi ya Mama Bikira Maria kwa mwanaye, Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa ufupi Lengo Kuu la Legio ya Maria ni kufanya kazi ya kupigana vita vya yule mwovu shetani ili kutakatifuza malimwengu ndani ya wanachama na jamii inayotuzunguka. - KAZI ZINAZOFANYIKA:
Kusaidiana na Kanisa Katoliki mahalia ili kuwasaidia wenye shida mbalimbali za kiroho na kimwili, kuwafariji na kuwapa moyo ili wasikate tamaa katika kumtegemea Mungu na kuishi maisha ya uchaji wa Mungu bila kuchoka.
Walegio pia hufanya bidii katika kutembelea wagonjwa Hospitalini na majumbani, kuwafariji wafiwa katika familia zao kwa sala na NENO la Mungu.
Kutekeleza maelekezo yanayotolewa na uongozi Hairakia na pia Halmashauri ya Walei Parokia pamoja na Uongozi wa ngazi za juu wa Legio ya Maria.
- MATARAJIO:
- Kuimarisha wana Utume kwa Semina mbalimbali za kiroho pamoja na Elimu ya jamii.
- Kuhamasisha wana Parokia kupitia Jumuiya zilizopo ili wengi waweze kuufahamu utume na kujiunga. Lengo likiwa ni kuwa na Jeshi kubwa litakalokuwa tayari kupigana na yule mwovu shetani na hatimaye kuwa washindi.
- HITIMISHO:
Legio maana yake ni Jeshi (Legion), hivyo Walejio wote ni Wanajeshi wakiongozwa na Mama Bikira Maria katika vita vya kumng’oa Ibilisi na Jeshi lake ili ulimwengu utakatifuzwe.
Hivyo walegio ya Maria wapo tayari kupigana vita hivyo hadi mwisho wa nyakati zao. Tunaomba Mungu aendelee kututia nguvu. Amina.