event, Matukio, wawata

SEMINA YA WAWATA PAROKIA TAREHE 04/05/2024

MADA: IMANI

MTOA MADA: PD. PASCHAL DIONIS – SJ

KARIBU.

Maana ya Imani______________________________

Ili kuwa na Imani thabiti tunahitaji

  1. Kuwa tayari kuchukua mwelekeo ambao Mungu anataka tuelekee.
  2. Kushirikisha yale yote ambayo Mungu ametupa.
  3. Kuwa tayari kupokea mateso kama Mungu ataruhusu yaani kuwa wavumilivu.
  4. Kutafuta Muungano na Mungu katika Sala, ndiyo kuwa mtu aliyesimama katika masuala ya kiroho.
  5. Moyo wa shukrani na sifa kwa Mungu, tukinukuu namna Bikira Maria alivyosema katika LK 1:46-47 “Moyo wangu wamtukuza Bwana na Roho yangu yamwazimisha Bwana”.
  6. Kuyatunza yote mazuri na mabaya tuliyopitia japo mengine ni ya kukuumiza.
  7. Kuwa na uwezo wa kusimama chini ya Msalaba ili kumwambia Yesu Mwokozi wetu yale yote tunayohitaji katika Maisha yetu.
  8. Sala tukikumbuka na kushuhudia namna Mama Bikira Maria alivyosali akimsubiri Roho Mtakatifu.

TAFAKARI

Ni nini Mapenzi ya Mungu katika Maisha yako?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *