Uncategorized

MATANGAZO YA JUMAPILI YA MATAWI MWAKA ‘C’– 13/04/2025

  1. Ratiba ya maungamo kwa Juma Kuu inapatikana katika ubao wa matangazo.  Waamini mnaombwa kuipitia. Kutakuwa na mapadri wageni watakaoungana na mapadri wa hapa kuungamisha.  
  • T-Sheti za Jubilei na Upadrisho zinapatikana katika duka la VIWATA kwa bei ya Sh. 10,000, 15,000 na 20,000.
  • Alhamisi Kuu Misa itaanza saa 10:30 jioni.  Ibada ya kuabudu itaanza saa 1:00 usiku, na Kanda zitakazoanza ni YERIKO na GALILAYA. Ratiba nzima ya kuabudu inapatikana katika ubao wa matangazo.
  • Utaratibu wa Njia ya Msalaba siku ya Ijumaa Kuu ni kama ifuatavyo:-  Maandamano ya njia ya Msalaba yataanzia katika Kituo cha Mabradha wa Upendo-karibu na Chuo cha Mipango kuja kanisani hapa kupitia geti kuu la mbele la kanisa. Waamini mnahimizwa kushiriki.  
  • Ibada ya Ijumaa Kuu itaanza saa 9:00 alasiri.  Jumamosi Misa ya Mkesha itaanza saa 3:00 usiku.
  • Jumapili 20/4/2025 siku ya Pasaka Misa zitakuwa kama kawaida: Misa ya Kwanza itakuwa saa 12:00 asubuhi, Misa ya Pili itaanza saa 1:00 asubuhi, Misa ya tatu itakuwa saa 3:00 asubuhi na Misa ya watoto itakuwa saa 5:00 asubuhi na Misa ya Kiingereza itakuwa saa 4:00 asubuhi.
  • Jumatatu ya Pasaka kutakuwa na Misa mbili.  Misa ya Kwanza saa 12:30 asubuhi na Misa ya Ubatizo wa watoto itaanza saa 2:30 asubuhi.
  • Tarehe 15/04/2025 kutakuwa na Misa ya kubariki Mafuta ya KRISMA. Misa itaanza saa 4:00 asubuhi Kanisa Kuu. Waamini ambao wangependa kushiriki Misa hiyo wanakaribishwa.
  • Vijana Wamisionari watakuwa na Semina kuanzia tarehe 25/4/2025 na 26/4/2025 semina itafanyika katika ukumbi wa Inyasa kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi na saa 8:00 – 10:00 jioni michezo katika uwanja wa Sheli.
  1. Waamini wote waliochukua Bahasha za Kwaresma mnaombwa kuzirudisha. Mwisho wa kurudisha Bahasha hizo ni tarehe 18/04/2025 wiki Kuu. Waamini mnakumbushwa kutumbukiza bahasha hizo kwenye masanduku ya sadaka.
  1. Jumatatu tarehe 14/4/2025 hadi Jumatano tarehe 16/4/2025 kutakuwa na Semina ya tafakari ya Juma Kuu itakayoanza saa 10:00 hadi saa 12:30 jioni katika ukumbi wa Inyasi. Waamini wote mnahimizwa kushiriki.
  1. Viongozi wote wa Kanda mnaombwa kufika Parokiani Jumatatu tarehe 14/4/2025 saa 10:00 jioni kuonyeshwa vituo vya Njia ya Msalaba mtakavyosimamia Ijumaa Kuu. Pia sala ya kutumia Jumuiyani Ijumaa Kuu inapatikana kwenye viboksi katka Jengo la Halmashauri ya walei. Viongozi wa Jumuiya mnaombwa kuzichukua.
  1. Tunawashukuru Jumuiya ya MT. PETER CLAVERY  na  MT. BERNADETHA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. PETRO MTUME na (B) MT. MAXIMILIAN KOLBE.  Wafuatao wajiandae kuhudumu JumaKuu, Alhamisi Kuu WAWATA na Moyo Mt. Wa Yesu, Ijumaa Kuu Uwaka na Viwawa, Jumamosi Mkesha Uwaka na Kamati ya Ulinzi, Jumapili ya Pasaka Jumuiya ya MT. GABRIEL MALAIKA MKUU  na MT. JEAN MARIA MUZEEY, jumatatu ya Pasaka Utume wa Fatima na Legio Maria.
  1. NDOA.
  2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Albert Hilu, wazazi wake ni Antony Nginwa na Monica Makeja anataka kufunga ndoa na Agatha Nganga, wazazi wake ni Celestine Nganga na Zena Mbaraka.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Justine Israel, wazazi wake ni Israel Silayo na Frola Silayo anataka kufunga ndoa na Ester Mussa, wazazi wake ni Mussa Mnyanduli na Yunisi Henry.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Silvanus Chistian, wazazi wake ni Christian Mapunda na Agnes Moyo anataka kufunga ndoa na Velian Venance, wazazi wake ni Venance Kigwinya na Mailes Luziro.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Aloyce Joseph, wazazi wake ni Joseph Musuluza na Lucy Mchiwa anataka kufunga ndoa na Rachel Henry, wazazi wake ni Henry Mazengo na Peris Jonathan.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Evaristo Ignas, wazazi wake ni Ignas Kasila na Juliana Simon anataka kufunga ndoa na Kezia Michael, wazazi wake ni Michael Paulo na Rozi Yako.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish, FACEBOOK: Parokia Ya Kndege, INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *