MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINIKA YA UTATU MTAKATIFU MWAKA ‘C’– 15/06/2025

  1. Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kuwasilisha mchango wa sherehe ya upadrisho; na waamini waliochukua kadi na fomu za mchango huo mnaombwa pia kuwasilisha mchango huo.  Tunawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa michango yao. Tunawashukuru Jumuiya ya Mt. Magreth Maria Alacoque, John De Brito, Utume wa Rita wa Kashia, utume wa wasoma masomo, Mt. Nicholaus Owen, Mt. Paulo Miki, Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Mt. Augustino, Mt. Mikael Malaika Mkuu, na Mt Monica  kwa kumaliza mchango wao kwa wakati, pia Jumuiya za Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Bikira Maria Mama Wa Kanisa na Mt. Yosefu Mfanyakazi kwa kumaliza michango na kuvuka lengo.
  • Jumamosi tarehe 21/06/2025 kutakuwa na Mkutano wa H/Walei Parokia utakaofanyika saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Inyasi. Viongozi wa Jumuiya na wenyeviti wa vyama vya kitume ngazi ya Parokia mnasisitizwa kuhudhuria mkutano huu bila kukosa. Pia mnaombwa kuchua ajenda  za mwaliko wa mkutano getini.
  • Alhamisi tarehe 19/06/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya SAMARIA. Alhamisi  ijayo tarehe 19/06/2025 wajiandae Kanda ya GALILAYA.Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
  • Viongozi mnaombwa kurejesha fomu za sensa 2025 katika ofisi ya mratibu wa Halmashauri ya Walei Parokia.
  • Mafundisho ya ndoa yatakuwa tarehe 20 – 22/06/2025 hapa Parokiani.
  • Dominika ijayo ni sherehe ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo. Kutakuwa na misa tatu tu. Ya kwanza saa 12:00 asubuhi, ya pili saa 01:00 asubuhi, na ya tatu saa 03:00 asubuhi ikifuatiwa na maandamano ya Ekaristi Takatifu. Aidha katika misa hiyo ya tatu watoto watapokea sakramenti ya Komunyo ya Kwanza.
  • Maungamo kwa watoto watakaopokea Komunyo ya Kwanza tarehe 22/06/2025 yatakuwa Ijumaa ijayo tarehe 20/05/2025 kuanzia saa 03:00 asubuhi hadi saa sita na nusu mchana, na saa 10:00 hadi saa 12:00 jioni.
  • Waamini mnaombwa kuleta maua ya asili ( yaliyochanua ) siku ya Ijumaa na Jumamosi kwa ajili ya Ekaristi Takatifu.
  • Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limeandaa vipeperushi vya elimu ya uraia kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge 2025. Waamini mnahimizwa kuchukua vipeperushi vya elimu hiyo katika viboksi nje ya milango ya Kanisa kwa ajili ya kujisomea.  
  1. Viongozi wa Jumuiya zifuatazo mnaombwa kufika siku ya Jumatano saa 11:00 Jioni katika Ofisi ya Halmashauli ya Walei Parokia kwa ajili ya Kikao cha maandalizi ya maandamano ya Ekaristi Takatifu: Mt. Stephano, Mt. Yohane wa Msalaba, Mt. Simone Zelote, Mt. Maximillian Kolbe, Mt. Bernadetha, Mt. Clara wa Assis, Mt. Gabriel Malaika Mkuu, Mt. Francis wa Assisi, Mt. Theresia wa Avila na Mt. Monica.
  1. Tunawashukuru Jumuiya ya MT. KATARINA WA SIENA   na utume wa Karismatiki Katoliki kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada.  Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. THERESA WA MTOTO YESU na (B) MT. FRANCIS WA ASSISI.  Jumuiya ya MT. PETER FEBER na MT. JOSEFU MFANYA KAZI wajiandae.
  1. NDOA.

        h)   Kwa mara ya Kwaza: Ndg. Msafiri Robert Mashauri, wazazi wake ni Robert Mashauri na Suzana

               Elias anataka kufunga ndoa na Lukresia Martin Dugu, wazazi wake ni Martin Dugu na Martha

               Nyamisi.

  1. Kwa mara ya Pili: Ndg. David Chalahan, wazazi wake ni Chalahan Malima na Agnes Dabu anataka kufunga ndoa na Levina Christopher, wazazi wake ni Christopher Tarimo na Akwilina Tesha.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Peter Eliud, wazazi wake ni Eliud Ndidi  na Paulina Ndidi anataka kufunga ndoa na Regina Blastus, wazazi wake ni Blastus Joseph na Lucy Sunyai.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. James Juma, wazazi wake ni Juma Stima na Jane Paulo anataka kufunga ndoa na Angela William, wazazi wake ni William Mark na Elizabeth Karol.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Fortunatus Roman, wazazi wake ni Roman Jackob na Salvina Msati anataka kufunga ndoa na Maria Nishima, wazazi wake ni Blengo Mwikola na Anna Chisanza.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Antony Mwalyambi, wazazi wake ni Leonard Mwalyambi na Justina John anataka kufunga ndoa na Maria Rhobi, wazazi wake ni Augustine Rhimo na Juliana Rhimo.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. George Elias, wazazi wake ni Elias Joseph na Veis Mlee anataka kufunga ndoa na Patricia Respia, wazazi wake ni Respia Efrem na Felista Kleopha.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *