MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINIKA YA PASAKA MWAKA ‘C’– 20/04/2025

  1. T-Sheti za Jubilei na Upadrisho zinapatikana katika duka la VIWATA kwa bei ya Sh. 10,000, 15,000 na 20,000.
  • Ofisi ya Parokia itafungwa kuanzia tarehe 22/04/2025 hadi tarehe 29/04/2025.
  • Jumatatu ya Pasaka kutakuwa na Misa mbili.  Misa ya Kwanza saa 12:30 asubuhi na Misa ya Ubatizo wa watoto itaanza saa 2:30 asubuhi. Watahudumu Utume wa Fatima na Legio Maria.
  • Jumatatu tarehe 21.04.2025 kutakuwa na ibada maalum ya Pasaka ya dhehebu zote itakoyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 07:00 mchana. Waamini mnahimizwa kushiriki.  
  • Vijana Wamisionari watakuwa na Semina kuanzia tarehe 25/4/2025 na 26/4/2025. Semina itafanyika katika ukumbi wa Mt Inyasi kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi; na saa 8:00–10:00 jioni michezo katika uwanja wa Sheli.
  • Ijumaa tarehe 25/04/2025 kutakuwa na Mkesha wa kuupokea mwezi wa Bikira Maria. Mkesha utaanza saa 2:00 usiku na kuisha saa 12:00 asubuhi. Waamini wote mnahimizwa kushiriki.
  • Tunawashukuru Jumuiya ya MT. PAULO MTUME  na  MT. YOHANE WA MSALABA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada.  Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. GABRIEL MALAIKA MKUU na (B) MT. JEAN MARIA MUZEEY.  Jumuiya ya MT. CLARA WA ASISSI  na MT. MONICA, wajiandae.
  • NDOA.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Albert Hilu, wazazi wake ni Antony Nginwa na Monica Makeja anataka kufunga ndoa na Agatha Nganga, wazazi wake ni Celestine Nganga na Zena Mbaraka.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Justine Israel, wazazi wake ni Israel Silayo na Frola Silayo anataka kufunga ndoa na Ester Mussa, wazazi wake ni Mussa Mnyanduli na Yunisi Henry.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Silvanus Chistian, wazazi wake ni Christian Mapunda na Agnes Moyo anataka kufunga ndoa na Velian Venance, wazazi wake ni Venance Kigwinya na Mailes Luziro.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish, FACEBOOK: Parokia Ya Kndege, INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *