MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINIKA YA KUPAA KWA BWANA TAREHE 12/05/2024

                   MATANGAZO YA DOMINICA YA KUPAA BWANA MWAKA ‘B’– 12/05/2024

  1. Baba Paroko ameandaa Semina kwa waamini wote juu ya Mama Bikira Maria kila siku ya Ijumaa saa 10:00 jioni kwa kipindi chote cha mwezi wa tano.
  • Magazeti ya kiongozi na Enendeni yanapatikana hapo nje.
  • Mafundisho ya ndoa mwezi huu yatakuwa tarehe 17, 18, na 19. Wanaotarajia kufunga ndoa mnaombwa kujiandikisha ofisini.
  • Viongozi wote wa Jumuiya mnakumbushwa kufanya mikutano ya Jumuiya kuandaa mapendekezo ya Kanuni za Parokia kama ilivyoelekezwa na Halmashauri ya Walei.  Pia Viongozi wa Kanda mnakumbushwa kufuatilia na kuwasilisha mapendekezo hayo kwa wakati.
  • Jumamosi tarehe 18/05/2024 kutakuwa na Semina ya Wenyeviti/wasaidizi wa Jumuiya na Vyama vya Kitume. Semina itaanza saa 3:00 asubuhi hapa Parokiani.
  • Jumamosi tarehe 18/5/2024 kutakuwa na kikao cha wazazi na walezi wa watoto wa Ekaristi. Kikao kitaanza saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Inyasi.
  • Tunashukuru Jumuiya ya MT. YOHANE WA MSALABA  na MT. PAULO MTUME kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) KARISMATIKI KATOLIKI na (B) MT. THERESIA WA AVILLA.  Jumuiya ya MT. ANDREA BOBOLA  na KRISTU MFALME wajiandae.
  • NDOA. (SOMA MATANGAZO YA “KWA MARA YA KWANZA TU”)
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Frank Batholomeo, baba  yake ni Batholomeo Mvami na mama yake ni Iluminata John anataka kufunga ndoa na Eveline Lucas, baba yake ni Lucas Sugwa na mama yake ni Martha Magwegwe. Wote wanasali katika parokia ya Petro Mtume – Swaswa, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Denis Bonephace, baba  yake ni Bonephace Xavery na mama yake ni Faustina Kagemulo anataka kufunga ndoa na Theresia Augustino, baba yake ni Augustino Kabeluka na mama yake ni Ceoelina Kulwa. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Florence Philibert, baba  yake ni Philibert Semakula na mama yake ni Veneranda Kemilembe  anataka kufunga ndoa na Lucia Augustino, baba yake ni Augustino Mlinga na mama yake ni Agnes Faustine. Wote wanasali katika parokia ya Mt. Yoseph Mfanyakazi – Ihumwa, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Alphonce Kankila, baba  yake ni Kankila Watelusi na mama yake ni Sesilia Mwanang’ombe  anataka kufunga ndoa na Ester Zabron, baba yake ni Zabron Kalilo na mama yake ni Grace Nicholaus. Wote wanasali katika parokia ya Nkuhungu, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Erick Humphurey, baba  yake ni Humphurey Munisi na mama yake ni Zena Mtizi anataka kufunga ndoa na Maryagnes Lazaro, baba yake ni Lazaro Chuwa na mama yake ni Evarista Malya. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Basil Ndetembea, baba  yake ni Joseph Kirango na mama yake ni Antonia Simon anataka kufunga ndoa na Suzana Ernest, baba yake ni Ernest Muhemeli na mama yake ni Mkatale Sigani. Wote wanasali katika parokia ya Kristu Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Deogratias Mutekanga, baba  yake ni Charles Sililo na mama yake ni Leticia John anataka kufunga ndoa na Rozaria Sikuku, baba yake ni Stanslaus Dakho na mama yake ni Anastazia Daati. Wote wanasali katika Parokia ya Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Sebastian Mathias, baba  yake ni Mathias Lubinsha na mama yake ni Eva Lameck anataka kufunga ndoa na Jackline Adelbert, baba yake ni Adelbert Kakoko na mama yake ni Sophia Charles. Wote wanasali katika parokia ya St. Joseph Cathedral“, Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.
  1. Kwa mara ya Tatu: Ndg. Simoni Dara, baba  yake ni Joseph Masanja na mama yake ni Anna Simon anataka kufunga ndoa na Anna Gidion, baba yake ni Gidion Samwel na mama yake ni Janeth Kilahuzi. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege, Jimbo Kuu la Dodoma.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:parokiayakiwanjachandege.or.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *