- Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kuwasilisha mchango wa sherehe ya upadrisho; na waamini waliochukua kadi na fomu za mchango huo mnaombwa pia kuwasilisha mchango huo. Tunawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa michango yao. Tunawashukuru Jumuiya ya Mt. Stanslaus Kostika, Mt. David Lewis, Ursula, Jean Maria Muzeey, Wat. Joackim na Anna, Philip Evans na Mt. Maria Goreth kwa kumaliza mchango wao kwa wakati, pia Jumuiya za Mt. Kizito, Mt. Yohane wa Msalaba, Mt. Yuda Thadei, Mt. Alphonce Rodriguzi na Mt. Theresia wa Mtoto Yesu kwa kupunguza michango yao.
- Alhamisi tarehe 05/06/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya YERUSALEMU. Alhamisi ijayo tarehe 12/06/2025 wajiandae Kanda ya BETHLEHEMU.Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
- Waamini wote mnatangaziwa kuwa Jumapili tarehe 15/06/2025 tutakuwa na Harambee ya Pili kwa ajili ya kuchangia Sherehe ya Parokia, Upadrisho, na Uzinduzi wa Mwaka wa Jubilee. Mnaombwa kujiandaa vyema kumtolea Mungu kwa upendo ili kufikia malengo ya mahitaji ya Sherehe.
- Kwaya ya Mt. Gemma Galgani Parokia ya K/Ndege wanatarajia kuzindua Albam ya nyimbo za Sifa na Tafakari tarehe 15/06/2025. Uzinduzi utafanyika hapa Parokiani kwenye Misa zote. Wanaomba waamini muwaunge mkono.
- T-Sheti za wakubwa na watoto, vikoi, na vikombe vya Upadrisho na Sherehe ya Parokia vinapatikana nje katika duka la VIWATA.
- Tunawashukuru Jumuiya ya MOYO MTAKATIFU WA YESU na KRISTU MFALME kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) KARISMATIKI na (B) MT. KATARINA WA SIENA. Jumuiya ya MT. ANTONY DANIEL na MT. MARIA GORETI wajiandae.
- NDOA.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Fortunatus Roman, wazazi wake ni Roman Jackob na Salvina Msati anataka kufunga ndoa na Maria Nishima, wazazi wake ni Blengo Mwikola na Anna Chisanza.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Antony Mwalyambi, wazazi wake ni Leonard Mwalyambi na Justina John anataka kufunga ndoa na Maria Rhobi, wazazi wake ni Augustine Rhimo na Juliana Rhimo
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. George Elias, wazazi wake ni Elias Joseph na Veis Mlee anataka kufunga ndoa na Patricia Respia, wazazi wake ni Respia Efrem na Felista Kleopha.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Godfrey Medard, wazazi wake ni Medard Philbert na Frola Buyogera anataka kufunga ndoa na Subira Fred, wazazi wake ni Fred Mwasambili na Agatha Adolph.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Joseph Herman, wazazi wake ni Herman Matonya na Jenni Akida anataka kufunga ndoa na Advela Martine, wazazi wake ni Martine Mulumbula na Ziada Juma.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Nikodemu Filberth, wazazi wake ni Filberth Mwalongo na Jaker Mfyagisa anataka kufunga ndoa na Veneranda Mavanza, wazazi wake ni Augustino Mavanza na Theresia Bernard.
MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:
Parokiayakiwanjachandege.or.tz.
NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish
KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:
YOUTUBE: Kndege Parish
FACEBOOK: Parokia Ya Kndege
INSTAGRAM: Kndege_Parish