- Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kuwasilisha mchango wa sherehe ya upadrisho; na waamini waliochukua kadi na fomu za mchango huo mnaombwa pia kuwasilisha mchango huo. Tunawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa michango yao. Tunawashukuru Jumuiya ya Mt. Bernadetha, Mt. Yohane Paulo wa II na Mt. Alberto Hurtado kwa kumaliza mchango wao kwa wakati, pia Jumuiya za Mt. Antony Daniel, Mt. Francis Jerome, Mt. Andrea Bobola na Mt. Karoli Lwanga, Mt. Francis wa Asissi na B.M.T.L kwa kupunguza michango yao.
- Alhamisi tarehe 29/05/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya YUDEA. Alhamisi ijayo tarehe 05/06/2025 wajiandae Kanda ya YERUSALEMU.Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
- Waamini wote mliochukua bahasha za Radio Maria mnakumbushwa kuzirudisha leo. Pia kwa wale ambao hawakufanikiwa kuja nazo leo basi mnaombwa kuzileta Jumapili ijayo. Bahasha hizo zitumbukizwe kwenye masanduku ya sadaka. Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa pia kuwa matembezi ya Sanamu ya Mama yatahitimishwa 31/05/2025. Mnaombwa kukusanya hela zote za matembezi na kuziweka katika Akaunti ya Mkombozi Bank na CRDB na kukabidhi Bank Slip kwa Mweka hazina wa Parokia.
- Jumamosi tarehe 31/05/2025 kutakuwa na semina na sala kuanzia saa 10:00 jioni, na Jumapili 01/06/2025 baada ya misa ya tatu tutaendelea na semina na sala. Hii ni kwa ajili ya wanafamilia, watoto, wazee-babu na bibi. Nyote mnakaribishwa.
- Umoja wa Wafransisko Dodoma watakuwa na Hija tarehe 31/05/2025, saa 04:00 asubuhi. Maandamano yataanzia kwenye Fremu za Magereza Bahi Road kuelekea Kanisa Kuu.Waamini wote mnaalikwa kushiriki.
- Watu wazima waliobatizwa usiku kwenye mkesha wa Pasaka tarehe 19/04/2025 na watoto waliobatizwa tarehe21/04/2025 Jumatatu ya Pasaka, vyeti vyenu viko tayari. Mnatangaziwa kuvichukua kuanzia Jumanne katika Ofisi ya Parokia. Watakaokuja mwezi mmoja baada ya tangazo hili watatozwa faini ya Tsh 10,000/-
- Karismatiki Katoliki Jimbo Kuu Dodoma imeandaa Kongamano la Pentekoste litakalofanyika katika Kituo cha Kanaani Miyuji kuanzia tarehe 30.05.2025 hadi tarehe 08.05.2025. Wote mnakaribishwa.
- T-Sheti za wakubwa na watoto, vikoi, na vikombe vya Upadrisho na Sherehe ya Parokia vinapatikana nje katika duka la VIWATA.
- Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kurudisha bahasha za Pasaka. Mwisho wa kurudisha ni Jumannetarehe 27.05.2025.
- Tunawashukuru Jumuiya ya MT. ANDREA BOBOLA na MT. THERESIA WA AVILLA kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. GEMMA GALGAN na (B) MT. BIKIRA MARIA NYOTA YA ASUBUHI. Jumuiya ya KARISMATIKI na MT. KATARINA WA SIENA wajiandae.
- NDOA.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Godfrey Medard, wazazi wake ni Medard Philbert na Frola Buyogera anataka kufunga ndoa na Subira Fred, wazazi wake ni Fred Mwasambili na Agatha Adolph.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Joseph Herman, wazazi wake ni Herman Matonya na Jenni Akida anataka kufunga ndoa na Advela Martine, wazazi wake ni Martine Mulumbula na Ziada Juma.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Nikodemu Filberth, wazazi wake ni Filberth Mwalongo na Jaker Mfyagisa anataka kufunga ndoa na Veneranda Mavanza, wazazi wake ni Augustino Mavanza na Theresia Bernard.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Gerald Abdi, wazazi wake ni Seraphin Chaula na Zainabu Abdi anataka kufunga ndoa na Dorice Wankembeta, wazazi wake ni Audiphace Mushi na Mary Matika.
MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:
Parokiayakiwanjachandege.or.tz.
NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish
KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:
YOUTUBE: Kndege Parish
FACEBOOK: Parokia Ya Kndege
INSTAGRAM: Kndege_Parish