- Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kuwasilisha mchango wa sherehe ya upadrisho; na waamini waliochukua kadi na fomu za mchango huo mnaombwa pia kuwasilisha mchango huo. Tunawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa michango yao. Tunawashukuru Jumuiya ya Mt. Yoseph Mfanyakazi na Mt. Petro Mtume kwa kumaliza mchango wao kwa wakati, pia Jumuiya za Mt. Simoni Zelote, Mt. Josephine Bakitha, Mt. Karoli Lwanga na Mt. Bikira Maria Mama wa Kanisa kwa kupunguza michango yao.
- Alhamisi tarehe 22/05/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya NAZARETH. Alhamisi ijayo tarehe 29/05/2025 wajiandae Kanda ya YUDEA.Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
- Waamini wote mliochukua bahasha za Radio Maria mnatangaziwa kuzirudisha kuanzi Jumapili ya tarehe 25/5/2025. Bahasha hizo zitumbukizwe kwenye masanduku ya sadaka. Pia viongozi wa Jumuiya mnaombwa kukusanya hela zote za matembezi ya Mama na kuziweka katika Akaunti ya Mkombozi Bank na CRDB.
- Jumamosi tarehe 31/05/2025 kutakuwa na semina na sala kuanzia saa 10:00 jioni, na Jumapili 01/06/2025 baada ya misa ya tatu tutaendelea na semina na sala. Hii ni kwa ajili ya wanafamilia, watoto, wazee-babu na bibi. Nyote mnakaribishwa.
- Watu wazima waliobatizwa usiku kwenye mkesha wa Pasaka tarehe 19/04/2025 na watoto waliobatizwa tarehe21/04/2025 Jumatatu ya Pasaka, vyeti vyenu viko tayari. Mnatangaziwa kuvichukua kuanzia Jumanne katika Ofisi ya Parokia. Watakaokuja mwezi mmoja baada ya tangazo hili watatozwa faini ya Tsh 10,000/-
- T-Sheti za wakubwa na watoto, vikoi, na vikombe vya Upadrisho na Sherehe ya Parokia vinapatikana nje katika duka la VIWATA.
- Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kurudisha bahasha za Pasaka. Mwisho wa kurudisha ni Jumanne tarehe 27.05.2025.
- Tunawashukuru Jumuiya ya MT. ALPHONCE RODRIGUEZ na MT. AUGUSTINO kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MOYO MTAKATIFU WA YESU na (B) KRISTU MFALME. Jumuiya ya MT. GEMMA GALGAN na BIKIRA MARIA NYOTA YA ASUBUHI, wajiandae.
- NDOA.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Gerald Abdi, wazazi wake ni Seraphin Chaula na Zainabu Abdi anataka kufunga ndoa na Dorice Wankembeta, wazazi wake ni Audiphace Mushi na Mary Matika.
MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:
Parokiayakiwanjachandege.or.tz.
NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish
KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:
YOUTUBE: Kndege Parish
FACEBOOK: Parokia Ya Kndege
INSTAGRAM: Kndege_Parish