Uncategorized

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 5 YA KWARESIMA MWAKA ‘C’– 06/04/2025

  1. Jumla Kuu ya Fungu la Kumi mwezi wa Tatu tumekusanya kiasi cha Tsh. 39,322,650/=

Paroko anawashukuru waamini wote waliotoa Zaka ya mwezi wa Tatu. Mungu awabariki nyote.

  • Wazazi au walezi na wasimamizi wa watoto wachanga watakaobatizwa tarehe 21/4/2025, mnatangaziwa kuwa kutakuwa na semina siku ya Jumamosi tarehe 12/4/2025 saa 3:00 asubuhi hapa Parokiani katika ukumbi wa Inyasi.
  • Waamini wote tunatangaziwa kuwa kuanzia tarehe 24 – 29/06/2025 kutakuwa na Kongamano la Pili la Utoto Mtakatifu Kanda ya Kati yaani majimbo ya Dodoma, Singida na Kondoa (DOSIKO). Waamini mnaombwa kuwawezesha watoto wetu kadiri ya barua zilizofika Jumuiyani.
  • Tarehe 15/04/2025 kutakuwa na Misa ya kubariki Mafuta ya KRISMA. Misa itaanza saa 4:00 asubuhi Kanisa Kuu. Waamini ambao wangependa kushiriki Misa hiyo wanakaribishwa.
  • Waamini wote waliochukua Bahasha za Kwaresma mnaombwa kuzirudisha. Mwisho wa kurudisha Bahasha hizo ni tarehe 18/04/2025 wiki Kuu. Waamini mnakumbushwa kutumbukiza bahasha hizo kwenye masanduku ya sadaka.
  • Tarehe 13/04/2025 Jumapili ya MATAWI kutakuwa na Misa tatu:  Misa ya 1 ni saa 12:00 asubuhi; matawi yatabarikiwa Kanisani katika misa hii.  Misa ya II ni saa 1:30 asubuhi.  Matawi hayatabarikiwa katika Misa hiyo.  Misa ya III  itaanza kwa maandamano ya matawi yatakayoanzia Uwanja wa Vijana.  Waamini watakaoshiriki Misa ya II wataungana na wale wa Misa ya III kwa maandamano hayo yatakayoanza saa 3:30 asubuhi.  Hakutakuwa na Misa ya Watoto.
  • Jumatatu tarehe 14/4/2025 hadi Jumatano tarehe 16/4/2025 kutakuwa na Semina ya tafakari ya Juma Kuu itakayoanza saa 9:00 alasiri hadi saa 12:30 jioni katika ukumbi wa Inyasi. Waamini wote mnahimizwa kushiriki.
  • Ijumaa ijayo tarehe 11/04/2025 Njia ya Msalaba wataongoza KANDA yaYERIKO na Kwaya ya MT. AUGUSTINO pamoja na kutoa vipaji.
  • Alhamisi tarehe 10/04/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya VATICAN. Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
  1. Tunawashukuru Jumuiya ya MT. FRANCIS XAVERY  na  MT. NICHOLAUS OWEN  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. PAULO MTUME na (B) MT. YOHANE WA MSALABA.  Wafuatao wajiandae kuhudumu JumaKuu, Alhamisi Kuu WAWATA na Moyo Mt. Wa Yesu, Ijumaa Kuu Uwaka na Viwawa, Jumamosi Mkesha Uwaka na Kamati ya Ulinzi, Jumapili ya Pasaka Jumuiya ya MT. PETRO MTUME  na MT. MAXIMILIAN KOLBE, jumatatu ya Pasaka Utume wa Fatima na Legio Maria.
  1. NDOA.
  2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Justine Israel, wazazi wake ni Israel Silayo na Frola Silayo anataka kufunga ndoa na Ester Mussa, wazazi wake ni Mussa Mnyanduli na Yunisi Henry.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Aloyce Joseph, wazazi wake ni Joseph Musuluza na Lucy Mchiwa anataka kufunga ndoa na Rachel Henry, wazazi wake ni Henry Mazengo na Peris Jonathan.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Evaristo Ignas, wazazi wake ni Ignas Kasila na Juliana Simon anataka kufunga ndoa na Kezia Michael, wazazi wake ni Michael Paulo na Rozi Yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *