Uncategorized

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 4 YA KWARESIMA MWAKA ‘C’– 30/03/2025

  1. Wazazi au walezi mnatangaziwa kuwa mwisho wa kurudisha fomu za ubatizo wa watoto wachanga ni tarehe 3/4/2025. Pia mahojiano yatakuwa tarehe 4/4/2025 saa 03:00 asubuhi katika ukumbi wa Inyasi.
  • Ijumaa ijayo tarehe 04/04/2025 Njia ya Msalaba wataongoza KANDA yaGETHSEMAN na Kwaya ya MT. GEMA GALGAN pamoja na kutoa vipaji.KANDA ya YERIKO na Kwaya ya MT. AUGUSTINO wajiandae.
  • Ofisi ya Makatekista itaanza kuandikisha mafundisho ya wakatekumeni na watu wazima wasio na masakramenti mbalimbali kuanzia tarehe 01/04/2025.  
  • Waamini ambao wangependa kuchangia SHEREHE ya Parokia na UPADRISHO wanakaribishwa kuwasilisha michango yao katika Ofisi ya Paroko.  
  • Tarehe 05/04/2025 kutakuwa na mkutano wa Halmashauri ya Walei katika ukumbi wa Inyasi. Viongozi wa Jumuiya na vyama vya kitume mnaombwa kuwasilisha ajenda za mkutano huo katika ofisi ya H/Walei kabla ya tarehe 1/04/2025.  Viongozi wa Jumuiya na vyama vya kitume mnaombwa kuchukua nyaraka za mkutano huo hapo getini mzisome na kuzijadili.
  • Vyama vya Kitume vya sala na WAWATA mnakumbushwa kuhudhuria semina na misa yenu Jumamosi ya kwanza ya mwezi.
  • Uongozi wa Vijana na Mt. Rita unawaalika waamini wote kwenye hija iliyoandaliwa Mwanza kuanzia tarehe 15-18/5/2025. Gharama kwa mshiriki ni Sh. 100,000/- Kwa wale wanaopenda kushiriki pamoja na kuchangia safari hii wanaalikwa.
  • Alhamisi tarehe 03/04/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya YERUSALEMU na GALILAYA. Alhamisi  ijayo tarehe 10/04/2025 wajiandae Kanda ya VATICAN.Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
  • Tunawashukuru Jumuiya ya MT. ANTONY WA PADUA  na  MT. YUDA THADEI  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. PETER CLAVERY  CHAMWINO na (B) MT. BERNADETHA Jumuiya ya MT. PAULO MTUME  na MT. YOHANE WA MSALABA wajiandae.
  1. NDOA.
  2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Aloyce Joseph, wazazi wake ni Joseph Musuluza na Lucy Mchiwa anataka kufunga ndoa na Rachel Henry, wazazi wake ni Henry Mazengo na Peris Jonathan.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Evaristo Ignas, wazazi wake ni Ignas Kasila na Juliana Simon anataka kufunga ndoa na Kezia Michael, wazazi wake ni Michael Paulo na Rozi Yako.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish, FACEBOOK: Parokia Ya Kndege, INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *