MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 4 PASAKA MWAKA ‘C’– 11/05/2025

  1. Mafundisho ya ndoa kwa wanandoa watarajiwa yatakuwa tarehe 16–18/05/2025 hapa Parokiani.
  • Kutakuwa na mafundisho na mafungo ya Mazoezi ya Kiroho ya Mt Inyasi wa Loyola yatakayoanza leo saa tano kamili asubuhi katika ukumbi wa Parokia. Mazoezi haya yataangazia maisha binafsi, ndoa na familia, kazi, mahusiano, tabia, na miito. Waamini wote mnahimizwa kushiriki.
  • Viongozi wa Jumuiya mnatangaziwa kuwa kuanzia Jumamosi tarehe 17/05/2025 hadi 07/06/2025 waseminishaji watakuja jumuiyani kufundisha kuhusu kumjua Mungu kwa msaada wa Roho Mtakatifu.  Viongozi mnaombwa kuwasiliana na waseminishaji waliopangwa na kutenga muda wa kutosha kwa ajili ya semina.  Ratiba inapatikana katika ubao wa Matangazo.
  • Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kuwasilisha mchango wa sherehe ya upadrisho; na waamini waliochukua kadi na fomu za mchango huo mnaombwa pia kuwasilisha mchango huo.  Tunawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa michango yao. Tunawashukuru Jumuiya ya Mt. Pio na Mt. Jean Maria Muzeey  kwa kumaliza mchango wao kwa wakati, pia Jumuiya za Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Mt. Andrea Bobola, Mt. Stephano  na Mt. Josephine Bakitha kwa kupunguza michango yao.
  • Viongozi wa Jumuiya mnaombwa kuleta Sensa ya Mwaka 2025. Fomu zinapatikana kwa Katibu Mtendaji wa H/Walei. Jumuiya ambazo hazijarejesha Mpango kazi wa Mwaka 2025 mnaombwa kuurejesha katika Ofisi ya H/Walei.
  • T-Sheti za wakubwa na watoto, vikoi, na vikombe vya Upadrisho na Sherehe ya Parokia vinapatikana nje katika duka la VIWATA.
  • Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kutoa mchango wa Kongamano la Utoto Mt. Kanda (DOSIKO). Kila Jumuiya itoe kiasi cha 130,000/= kwa kila mshiriki kadri ya barua ilivyoelekeza.  Mwisho wa kuwasilisha michango hiyo ni tarehe 15/05/2025.
  • Tunawashukuru Jumuiya ya MT. CLARA WA ASISSI  na  MT. MONICA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada.  Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. ANDREA BOBOLA na (B) MT. THERESIA WA AVILLA.  Jumuiya ya MOYO MTAKATIFU WA YESU  na KRISTU MFALME, wajiandae.
  • NDOA.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Gerald Abdi, wazazi wake ni Seraphin Chaula na Zainabu Abdi anataka kufunga ndoa na Dorice Wankembeta, wazazi wake ni Audiphace Mushi na Mary Matika.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *