Uncategorized

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 4 MWAKA ‘C’– 02/02/2025

  1. Viongozi wa Jumuiya mnaombwa kurudisha bahasha za Krismasi; mwisho wa kurudisha bahasha hizo ni tarehe 9/2/2025.
  • Jumapili tarehe 9/2/2025 kutakuwa na mkutano wa VIWAWA katika ukumbi wa Inyasi mara baada ya misa ya tatu. VIWAWA wote mnaombwa kushiriki.
  • Wazazi wa watoto waliobatizwa tarehe 26/12/2024 mnaombwa kuchukua vyeti vyenu katika ofisi ya Parokia. Atakayekuja baada ya mwezi mmoja atalipa faini ya Tsh 10,000/-
  • Leo kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu hapa Parokiani kama mlivyotangaziwa Jumapili iliyopita. Waamini mnaombwa kujitokeza kwa wingi.
  • Uongozi wa Utume wa Familia ya Maridhiano Jimbo Kuu Katoliki Dodoma umeandaa Kliniki ya Ndoa na sherehe kwa wanandoa wenye kumbukizi za Ndoa kuanzia miaka 25,30,45 na 50 kwa heshima ya Mt. Valentino itakayofanyika Ijumaa tarehe 14/02/2025. Mchango kwa mshiriki mmoja ni Tsh. 25,000/= Sherehe itaanza na Misa takatifu saa 11:30 jioni ikifuatiwa na mashangilio mbalimbali katika ukumbi wa Roma Complex, Jimboni. Kwa maelezo zaidi tazama tangazo katika ubao wa matangazo.
  • Tunawashukuru Jumuiya ya MT. PIO  na  MT. JOHN DE BRITO  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. ROBERT BELLARMINE na (B) MT. SIMONI ZELOTE.  Jumuiya ya MT. STANSLAUS KOSTIKA  na MT. KIZITO wajiandae.
  • NDOA.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Blasius August, wazazi wake ni August John na Catherine Mathias anataka kufunga ndoa na Carolina Shukuru, wazazi wake ni Fanuel Mamadi na Martha Alfonsi.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Remmy Matembele, wazazi wake ni Matembele na Maria Lucas anataka kufunga ndoa na Upendo Hamisi, wazazi wake ni Hamisi Mnyang’walo na Selina Medhack.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Michael Adelio, wazazi wake ni Adelio Chalamila na Agnes Thomas anataka kufunga ndoa na Agnes Donald, wazazi wake ni Donald Charwe na Roda Chacha.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *