- Jumla kuu ya Fungu la kumi mwezi wa Nne (4) tumekusanya kiasi cha Tsh. 20,484,098/=
Paroko anawashukuru waumini wote waliotoa zaka ya mwezi wa Nne. Mungu awabariki nyote.
- Watu wazima wasio na Masakramenti mbalimbali pamoja na wakatekumeni mnatangaziwa kuwa mwisho wakuandikishwa ni 09/05/2025. Watakaochelewa wataandkishwa mwezi wa kumi.
- Kwaya ya Maria Mama wa Mungu inawaalika waamini wote kujipatia Flash za nyimbo za Maria katika Mwezi huu wa Mama. Flash zinapatikana hapo nje.
- Waamini mnatangaziwa kuwa mwezi huu wa Mama Bikira Maria kutakuwa na sala ya Rozari kila siku saa 11:00 jioni. Pia Alhamisi na Ijumaa saa 10:00 jioni kutakuwa na semina kuhusu Mama Bikira Maria.
- Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kuwasilisha mchango wa sherehe ya upadrisho kama mlivyopangiwa; na waamini waliochukua kadi na fomu za mchango huo mnaombwa pia kuwasilisha mchango huo. Tunawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa michango yao. Tunawashukuru Jumuiya ya Mt. Francis Borgia kwa kumaliza mchango wao kwa wakati, pia Jumuiya za Mt. Simoni Zelote, Mt. Karoli Lwanga na Mt. Yoseph Mfanyakazi kwa kupunguza michango yao.
- Viongozi wa Jumuiya mnaombwa kuleta Sensa ya Mwaka 2025. Fomu zinapatikana kwa Katibu Mtendaji wa H/Walei. Jumuiya ambazo hazijarejesha Mpango kazi wa Mwaka 2025 mnaombwa kuurejesha katika Ofisi ya H/Walei.
- T-Sheti za wakubwa na watoto, vikoi, na vikombe vya Upadrisho na Sherehe ya Parokia vinapatikana nje katika duka la VIWATA.
- Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kutoa mchango wa Kongamano la Utoto Mt. Kanda (DOSIKO). Kila Jumuiya itoe kiasi cha 130,000/= kwa kila mshiriki kadri ya barua ilivyoelekeza. Mwisho wa kuwasilisha michango hiyo ni tarehe 15/05/2025.
- Tunawashukuru Jumuiya ya MT. GABRIEL MALAIKA MKUU na MT. JEAN MARIA MUZEEY kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. ALPHONSUS RODRIGUEZ na (B) MT. AUGUSTINO. Jumuiya ya MT. ANDREA BOBOLA na MT. THERESIA WA AVILLA, wajiandae.
MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:
Parokiayakiwanjachandege.or.tz.
NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish
KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:
YOUTUBE: Kndege Parish
FACEBOOK: Parokia Ya Kndege
INSTAGRAM: Kndege_Parish