Uncategorized

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 3 MWAKA ‘C’– 26/01/2025

  1. Viongozi wa Jumuiya mnaombwa kurudisha bahasha za Krismasi; mwisho wa kurudisha bahasha hizo ni tarehe 9/2/2025.
  • Wazazi wa watoto waliobatizwa tarehe 26/12/2024 mnaombwa kuchukua vyeti vyenu katika ofisi ya Parokia kuanzia Jumanne. Atakayekuja baada ya mwezi mmoja atalipa faini ya Tsh 10,000/-
  • Kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu Jumapili ya tarehe 02/02/2025 hapa Parokiani. Waamini mnaombwa kujitokeza  kwa wingi.
  • Uongozi wa Utume wa Familia ya Maridhiano Jimbo Kuu Katoliki Dodoma umeandaa Kliniki ya Ndoa na sherehe kwa wanandoa wenye kumbukizi za Ndoa kuanzia miaka 25,30,45 na 50 kwa heshima ya Mt. Valentino itakayofanyika Ijumaa tarehe 14/02/2025. Mchango kwa mshiriki mmoja ni Tsh. 25,000/= Sherehe itaanza na Misa takatifu saa 11:30 jioni ikifuatiwa na mashangilio mbalimbali katika ukumbi wa Roma Complex, Jimboni. Kwa maelezo zaidi tazama tangazo katika ubao wa matangazo.
  • Tunawashukuru Jumuiya ya MT. ALOYCE GONZAGA  na  MT. JOSEPHINE BAKITHA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. MAGRETH MARIA ALACOQUE na (B) MT. AGATHA.  Jumuiya ya MT. ROBERT BELLARMINE  na MT. SIMONI ZELOTE wajiandae.
  • NDOA.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Blasius August, wazazi wake ni August John na Catherine Mathias anataka kufunga ndoa na Carolina Shukuru, wazazi wake ni Fanuel Mamadi na Martha Alfonsi.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Remmy Matembele, wazazi wake ni Matembele na Maria Lucas anataka kufunga ndoa na Upendo Hamisi, wazazi wake ni Hamisi Mnyang’walo na Selina Medhack.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Michael Adelio, wazazi wake ni Adelio Chalamila na Agnes Thomas anataka kufunga ndoa na Agnes Donald, wazazi wake ni Donald Charwe na Roda Chacha.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Frank Sebastian, wazazi wake ni Sebastian Masinde na Noela Manyama anataka kufunga ndoa na Roziana Eliutha, wazazi wake ni Eliutha Chuhila na Flora Mgidange.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *