- Tarehe 21/03/2025 siku ya Ijumaa, Njia ya Msalaba wataongoza KANDA yaGALILAYA, na Kwaya ya MT. MARIA MAMA WA MUNGU, pamoja na kutoa vipaji.KANDA ya SAMARIA na YUDEA na Kwaya ya B.M.T.L wajiandae.
- Mafundisho ya ndoa kwa wanandoa watarajiwa yatakuwa tarehe 21-23/03/2025 hapa Parokiani.
- Kanuni za usimamizi na uendeshaji wa Parokia zinapatikana Duka la WAWATA kwa gharama ya Sh. 10,000/=
- Tarehe 22/03/2025 kutakuwa na semina ya waliofunga ndoa kuanzia mwezi mmoja hadi miaka 15. Semina itaanza saa 4:00 asubuhi.
- Wazazi/walezi mnatangaziwa kuchukua fomu za Ubatizo wa watoto wachanga katika Ofisi ya Parokia. Ubatizo utafanyika tarehe 21/04/2025 Jumatatu ya Pasaka. Viongozi wa Jumuiya wajaze sehemu zao na kupiga mhuri wa Jumuiya fomu hizo.
- Makatekista wamisionari wameandaa semina ya wanawake wote itakayofanyika Miyuji-Mbwanga kituo cha hija ( PODIUM) Jumapili tarehe 16/3/2025 kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 12:00 jioni. Wamama wote mnakaribishwa kupata majibu ya maswali yenu.
- Uongozi wa UWAKA Parokia wanawakumbusha wana UWAKA Jumuiya zote ambazo bado hawajalipa mchango wa Sh. 60,000/= za malezi ya Seminary ya Miyuji kulipa fedha hizo kabla ya tarehe 17/03/2025.
- Wana-UWAKA wote mnakumbushwa kuhudhuria ibada ya Mt. Yosefu siku ya Jumamosi tarehe 22/03/2025 itakayofanyika nyumba ya Malezi Seminari ya Miyuji.
- Kitaba kinachotoa mafunzo ya afya ya akili na magonjwa ya akili kama vile msongo wa mawazo, sonona, na magonjwa mengine yanayo husu afya ya akili kilicho andikwa na Ndugu Peter Njau kinapatikana getini kwa gharama ya Tsh. 6,000/=
- Alhamisi tarehe 20/03/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya BETHLEHEMU. Alhamisi ijayo tarehe 27/03/2025 wajiandae Kanda ya YERIKO.Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
- Tunawashukuru Jumuiya ya MT. RITA WA KASHIA na MT. KAROLI LWANGA kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. ANTONY WA PADUA na (B) MT. YUDA THADEI Jumuiya ya MT. FRANCIS XAVERY na MT. NICHOLAUS OWEN wajiandae.
- NDOA.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Denis Amani, wazazi wake ni Wilhard Joseph na Philotea Vumilia anataka kufunga ndoa na Nice Jackson, wazazi wake ni Jackson Massawe na Evaristina Leoni.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Gabriel Kitindi, wazazi wake ni Costantine Kitindi na Agnes Michael anataka kufunga ndoa na Neema Joab, wazazi wake ni Joab Thadayo na Maria Omary.
MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:
Parokiayakiwanjachandege.or.tz.
NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish
KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:
YOUTUBE: Kndege Parish
FACEBOOK: Parokia Ya Kndege, INSTAGRAM: Kndege_Parish