
- Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kuwa tarehe 07/07/2024 Siku ya sherehe ya Parokia tutamkabidhi Katekista Aidan zawadi ya shukrani kwa utume aliofanya parokiani. Hivyo michango ya kutoka Jumuiyani iwasilishwe kwa Mhazini wa Parokia Mapema. Mwisho ni siku ya Ijumaa tarehe 5/7/2024
- Jumapili ijayo tutakuwa na misa tatu tu: ya kwanza saa 12:00 asubuhi, ya pili saa 1:00 asubuhi na ya tatu saa 3:00 asubuhi.
- Wazazi na Walezi wa watoto wa Kipaimara mnatangaziwa kuwa Jumamosi tarehe 06/07/2024 kutakuwa na kikao hapa Parokiani katika ukumbi wa Inyasi saa 3:00 asubuhi.
- Wazazi na walezi mnaombwa kuchukua fomu za Ubatizo wa watoto wachanga utakaotakuwa tarehe 17/8/2024.
- Tarehe 2/7/2024 hadi tarehe 30/7/2024 Makatekista wataanza kuandikisha watoto wa mafundisho ya Kipaimara, Komnyo ya Kwanza na watu wazima wa masakiramenti mbalimbali.
- Kamati ya Hija Imeandaa safari ya Hija Kibeho Rwanda kuanzia tarehe 3/9/2024 hadi 10/9/2024. Safari hiyo itapitia Butiama kwa mtumishi wa Mungu Mwl. Julias Nyerere na Gharama ni 350,000/=
- Kwaya ya BMTL ikiungana na Kwaya Mbalimbali ikiwemo Kwaya kutoka Nchini Rwanda, inazindua uuzaji wa Tiketi za Tamasha la Ledochowska litakalofanyika ukumbi wa vijana tarehe 25/8/2024. Hivyo inawaomba waamini wote tununue tiketi kwa ajili ya kuimarisha utume.
- Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. MAGRETH MARIA ALACOQUE, MT. MARIA GORETI, MT. ALBERTO HURTADO, MT. BERNADETHA, MT. NICHOLAUS OWEN, MT. ANDREA KAGWA. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. ALPHONCE RODRIGUEZ, MT. KAROLI LWANGA, MT. ROBERT BELLARMINE, MT. ANTONY WA PADUA, MT. PAULO MIKI, MT. FRANCIS BORGIA.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
- Tunashukuru Jumuiya ya MT. ANTONY DANIEL na MT. MARIA GORETI kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. PETER FEBAR na (B) MT. YOSEPH MFANYAKAZI. Jumuiya ya MT. PAULO MIKI, na MT. MICHAEL MALAIKA MKUU wajiandae.
- NDOA. (SOMA MATANGAZO YA “KWA MARA YA KWANZA TU”)
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Mwita Vincent, baba yake ni Samson Chacha na mama yake ni Veronica Daniel anataka kufunga ndoa na Sarah Matika, baba yake ni Daniel Mwendi na mama yake ni Lois Julius. Bib Harusi mtarajiwa Alibatizwa Parokia ya K/Ndege na Bw. Harusi mtarajiwa anasali Parokia ya Familia Takatifu Nundu Jimbo kuu la Mwanza.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Fred Michael, baba yake ni Michael Ringo na mama yake ni Eliema Godmark anataka kufunga ndoa na Veronica Damiani, baba yake ni Damiani Muhono na mama yake ni Frorence Mshana. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Lameck Makoye, baba yake ni Sylivanus Gombanila na mama yake ni Clemencia Yamizi anataka kufunga ndoa na Irene Wunuo, baba yake ni Anderson Wunuo na mama yake ni Mary Shuma. Bw. Harusi Mtarajiwa anasali Parokia ya K/Ndege na Bi. Harusi Mtarajiwa anasali Parokia ya Mt. Kaloli Lwanga – Kahama.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Julius Juma, baba yake ni Emili Mafikiri na mama yake ni Lucresia Massawe anataka kufunga ndoa na Paulina Mtambalike, baba yake ni Willison Mtambalike na mama yake ni Immaculatha Sambi. Wote wanasali katika Kigango cha Mt. Peter Clever – Mlimwa C.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Paschal Anthony, baba yake ni Anthony Mdamu na mama yake ni Rufina Mwenda anataka kufunga ndoa na Rebecca Ezekiel, baba yake ni Ezekiel Chapote na mama yake ni Happiness Chapote. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Henrick Jordan, baba yake ni Jordan Tumbi na mama yake ni Avengelista Nyoni anataka kufunga ndoa na Faith Omar, baba yake ni Omar Rajab na mama yake ni Zainab Ally. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Claudio Damas, baba yake ni Damas Gabo na mama yake ni Felista Bukagu anataka kufunga ndoa na Anjelina Nyabenda, baba yake ni Nyabenda Paulo na mama yake ni Anastasia Amon. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. George Patrick, baba yake ni Patrick Kunambi na mama yake ni Magreth Vitalis anataka kufunga ndoa na Johaina Hassan, baba yake ni Hassan Hamis na mama yake ni Asha Rashid. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.
Pamoja na App ya parokia: KNDEGEPARISH
Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel yetu: KNDEGEPARISH
Facebook: PAROKIA YA KNDEGE
Waumini Mnaombwa KU-SUBSCRIBE