- Jumla Kuu ya Fungu la Kumi mwezi wa Pili tumekusanya kiasi cha Tsh. 30,256,397/=
Paroko anawashukuru waamini wote waliotoa zaka ya mwezi wa Pili. Mungu awabariki nyote.
- Tarehe 14/03/2025 siku ya Ijumaa, Njia ya Msalaba wataongoza KANDA yaYERUSALEMU na NAZARETH, na Kwaya ya MT. AUGUSTINO, pamoja na kutoa vipaji. KANDA ya GALILAYA na Kwaya ya MT. MARIA MAMA WA MUNGU wajiandae.
- Kanuni za usimamizi na uendeshaji wa Parokia zinapatikana Duka la WAWATA kwa gharama ya Sh. 10,000/=
- Wenyeviti wa Jumuiya na Vyama vya Kitume mnaombwa kuchukua Barua zenu kwenye Box la Barua Getini.
- Tarehe 15/03/2025 kutakuwa na Semina ya waweka hazina wa Jumuiya pamoja na wa Vyama vya Kitume ngazi ya Parokia. Semina itaanza saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Inyasi.
- Bahasha za Kwaresma bado zinapatikana katika stuli ndani ya Kanisa na kwenye viboksi nje ya Kanisa. Mnaporudisha bahasha mnaombwa kuzitumbukiza katika masanduku ya sadaka.
- Wazazi/walezi mnatangaziwa kuchukua fomu za Ubatizo wa watoto wachanga katika Ofisi ya Parokia. Ubatizo utafanyika tarehe 21/04/2025 Jumatatu ya Pasaka. Viongozi wa Jumuiya wajaze sehemu zao na kupiga mhuri wa Jumuiya fomu hizo.
- Kanisa dogo la kuabudia litafungwa kwa takribani wiki mbili kuanzia Jumanne ijayo kwa matengenezo. Wanaopenda kuabudu wataabudia katika kanisa kubwa mara baada ya misa za asubuhi hadi saa 12:30 jioni kwa siku za wiki. Jumapili ijayo waamini wanaweza kuabudu katika kanisa kubwa kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 12:30 jioni.
- Alhamisi tarehe 13/03/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya YUDEA. Alhamisi ijayo tarehe 20/03/2025 wajiandae Kanda ya BETHLEHEMU.Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
- Tunawashukuru Jumuiya ya MT. STEPHANO na MT. ALBERTO HURTADO kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. MARIA GORETH na (B) MT. ANDREA KAGWA Jumuiya ya MT. ANTONY WA PADUA na MT. YUDA THADEI wajiandae.
- NDOA.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Denis Amani, wazazi wake ni Wilhard Joseph na Philotea Vumilia anataka kufunga ndoa na Nice Jackson, wazazi wake ni Jackson Massawe na Evaristina Leoni.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Gabriel Kitindi, wazazi wake ni Costantine Kitindi na Agnes Michael anataka kufunga ndoa na Neema Joab, wazazi wake ni Joab Thadayo na Maria Omary.
MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:
Parokiayakiwanjachandege.or.tz.
NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish
KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:
YOUTUBE: Kndege Parish,
FACEBOOK: Parokia Ya Kndege,
INSTAGRAM: Kndege_Parish