MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA UTATU MTAKATIFU TAREHE 26/5/2024

                   

  1. Waumini mnakumbuswa kurudisha bahasha za fungu la Kumi na kuzitumbukiza kwenye masanduku ya sadaka.
  2. Magazeti ya kiongozi na Enendeni yanapatikana hapo nje.
  • Viongozi wote wa Jumuiya mnakumbushwa kufanya mikutano ya Jumuiya kuandaa mapendekezo ya Kanuni za Parokia kama ilivyoelekezwa na Halmashauri ya Walei. Pia Viongozi wa Kanda mnakumbushwa kufuatilia na kuwasilisha mapendekezo hayo. Jumamosi tarehe 1/6/2023 ni siku ya mwisho ya kuwasilisha mapendekezo hayo.
  • Jumuiya zinazohitaji kujaza nafasi za uongozi zilizo wazi zinaombwa kutoa taarifa kwenye ofisi ya H/Walei kufikia Jumamosi tarehe 1/6/2024 na uchaguzi utafanyika tarehe 8/6/2024.
  • Jumapili ijayo tarehe 2/06/2024 ni sherehe ya Mwili na Damu ya Kristo. Hivyo tutakuwa na misa tatu tu na baada ya misa ya tatu tutakuwa na maandamano ya Yesu wa Ekaristi. Watoto watapokea komunyo ya kwanza katika misa ya tatu na hakutakuwa na misa ya watoto.
  • Kamati tendaji za jumuiya zote za Kanda ya Galilaya watakuwa na Kikao na Kamati tendaji parokia siku ya Jumamosi tarehe 1 Juni 2024 saa 10:00 jioni.
  • Ijumaa Tarehe 31/5/2024 ni siku ya kufunga mwezi wa mama Bikira Maria. Misa itakuwa saa 11:00 jioni. Kabla ya misa kutakuwa na semina na sala ya Rozari kuanzia saa 10:00 kamili.
  • Viongozi wa Kanda wanakumbushwa kuwasilisha Sanamu za Bikira Maria pamoja na Sadaka zilizokusanywa Jumuiyani siku ya Ijumaa kwa mweka hazina wa parokia tarehe 31 Mei 2024 saa 9.00 Alasiri.
  • Leo ni siku ya kurejesha bahasha za Radio Maria. Wale wote waliochukua bahasha mnakumbushwa kurudisha na kuzitumbukiza katika masanduku ya sadaka. 
  1. Vijana wameandaa mkesha wa Mama Bikira Maria tarehe 30/5/2024 siku ya Alhamisi kuanzia saa 1:00 usiku hadi asubuhi hapa Parokiani. Wazazi tunaomba muwaruhusu vijana washiriki katika mkesha huo.
  1. Uongozi wa Uwaka Parokia unawaalika wanaume wote kuhudhurie Misa ya Shukrani itakayoadhimishwa na Baba Askofu Msaidizi. Misa itafanyika Kanisa Kuu tarehe 1/6/2024 saa 4:00 asubuhi.
  1. Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. ALPHONCE RODRIGUEZ, MT. KAROLI LWANGA, MT. ROBERT BELLARMINE, MT. PAULO MIKI, MT. FRANCIS BORGIA, MT. ANTONY WA PADUA. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. PETER CLAVER CHAMWINO, MT. AUGUSTINO, MT. GEMMA GALGAN, MT. MONICA, MT. ANTONY DANIEL, MT. DAVID LEWIS.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
  1. Tunashukuru Jumuiya ya MT. ANDREA BOBOLA  na MT. THERESIA WA AVILLA kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. PHILIP EVANS na (B) SHIRIKA LA MOYO MTAKATIFU WA YESU.  Jumuiya ya MT. GEMMA GALGAN,   na MT. BIKIRA MARIA NYOTA YA ASUBUHI wajiandae.
  1. NDOA. (SOMA MATANGAZO YA “KWA MARA YA KWANZA TU”)
  2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Godfrey Frumens, baba  yake ni Frumens Oswin na mama yake ni Zabibu Abuu anataka kufunga ndoa na Irene Costantin , baba yake ni Costantin Selestin na mama yake ni Caroline Ally. Wote wanasali katika parokia ya Mt. Polycarp– Misugusugu Pwani – Jimbo Kuu Katoliki la Dar-es-Salaam.
  • Kwa mara ya kwanza, Ndg Gaspar Gomora baba yake ni Gomora na mama yake ni Renada Kimulela anataka kufunga ndoa na Alida baba yake ni Innocent na mama yake ni Adventina Martine. Wote wanasali katika parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani, Kasumo, Jimbo la Kigoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Emmanuel Mchemwa, baba  yake ni Martin Luka na mama yake ni Margarita Njuu anataka kufunga ndoa na Balbina Victor, baba yake ni Victor Joseph na mama yake ni Luisa Palakata. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege– Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Oscar Kalinga, baba  yake ni Cassian Kalinga na mama yake ni Fatu Koga anataka kufunga ndoa na Margreth Haule, baba yake ni Walter Ngunguru na mama yake ni Maria Haule. Wote wanasali katika parokia ya Mafinga – Jimbo Katoliki la Iringa.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Kelvin Moris, baba  yake ni Moris Garigo na mama yake ni Flora Aloyo anataka kufunga ndoa na Fauster Alphonce, baba yake ni Alphonce Nyiridandi na mama yake ni Flavia Kazoba. Wote wanasali katika parokia ya Kinyerezi, Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Lucas Magacha, baba  yake ni Stephano Kikube na mama yake ni Annastazia Bhoke anataka kufunga ndoa na Lightness Emmanuel, baba yake ni Emmanuel Machiya na mama yake ni Clara Rashidi. Wote wanasali katika parokia ya B.M.M. wa Mwokozi Sinza, Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Michael Chota, baba  yake ni Jackson Machela na mama yake ni Estelina Kisenga anataka kufunga ndoa na Happy Kenan, baba yake ni Kenan Nkinela na mama yake ni Agnes Chanai. Wote wanasali katika parokia ya Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Frank Batholomeo, baba  yake ni Batholomeo Mvami na mama yake ni Iluminata John anataka kufunga ndoa na Eveline Lucas, baba yake ni Lucas Sugwa na mama yake ni Martha Magwegwe. Wote wanasali katika parokia ya Petro Mtume – Swaswa, Jimbo Kuu la Dodoma.
  1. Kwa mara ya Tatu: Ndg. Denis Bonephace, baba  yake ni Bonephace Xavery na mama yake ni Faustina Kagemulo anataka kufunga ndoa na Theresia Augustino, baba yake ni Augustino Kabeluka na mama yake ni Ceoelina Kulwa. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege, Jimbo Kuu la Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *