MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA 6 YA PASAKA MWAKA “B”

                  MATANGAZO YA DOMINICA YA 6 YA PASAKA MWAKA ‘B’– 05/05/2024

  1. Jumla kuu ya Fungu la kumi mwezi wa NNE tumekusanya kiasi cha Tsh. 26,508,571/=

*Tunawashukuru wote waliotoa kwa moyo wa ukarimu wakiwemo waliotoa kupitia mfumo wa sadaka dijital*

  • Makatekista wanaendelea kuandikisha mafundisho ya masakrament mbalimbali kama vile Ubatizo, Ekaristi na Kipaimara kwa watu wazima na watoto kuanzia miaka saba.
  • Wazazi na walezi mnatangaziwa kuwa watoto wa Mafundisho ya Ekaristi watafanya Mtihani tarehe 11/05/2024 siku ya Jumamosi saa 2:00 asubuhi. Wazazi muwahimize watoto wafike kwa wakati.
  • Baba Paroko ameandaa Semina kwa waamini wote juu ya Mama Bikira Maria kila siku ya Ijumaa saa 10:00 jioni kwa kipindi chote cha mwezi wa tano.
  • Leo Baada ya Misa viongozi wote wa jumuiya mnaombwa kupita katika meza ya Radio Maria hapo nje kwa ajili ya kuchukua bahasha za Mariathoni na kuzigawa kwa wanajumuiya.
  • Viongozi wa Kanda mnaombwa kuratibu matembezi ya sanamu za Bikira Maria zilizo tolewa kikanda
  • Leo mara baada ya Misa ya tatu kutakuwa na Semina ya Vijana katika ukumbi wa Inyasi. Vijana wote mnaombwa kuhudhuria.
  • WAWATA wanawatangazia viongozi wote wa Jumuiya kuwa wanaombwa kushiriki Baraka ya kutengeneza Sanamu ya Bikira Maria Msaada wa Wakristo. Pia zipo barua za ufafanuzi. Viongozi mnaombwa kuchukua barua hizo katika ofisi ya Wawata.
  • Jumapili tarehe 12/05/2024 kutakuwa na Misa mbili tu. Misa ya kwanza saa 12:00 asubuhi na Misa ya Pili saa 1:00 asubuhi. Misa ya uasikofusio itaanza saa tatu asubuhi katika kituo cha Hija, huko mbwanga.
  1. Magazeti ya kiongozi na Enendeni yanapatikana hapo nje.
  1. Jumuiya za zamu mnaombwa kuleta vibaji vya chakula zaidi, kama Unga wa ugali, unga wa ngano, sukari, mchele, maharage na vingine ili tusaidie wahitaji wa parokia.
  1. Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. STANSLAUS KOSTIKA, MT. FRANCIS JEROME, MT. AGATHA, KRISTU MFALME, MT. JEAN MARIA MUZEEY, MOYO MTAKATIFU WA YESU. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. MAGRETH MARIA ALACOQUE, MT. MARIA GORETI, MT. ALBERTO HURTADO, MT. BERNADETHA, MT. NICHOLAUS OWEN, MT. ANDREA KAGWA.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
  1. Tunashukuru Jumuiya ya MT. CLARA WA ASISSI  na MT. MONICA kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya Jumuiya ya (A) MT. ALPHONCE RODRIGUEZ  na (B) MT. AUGUSTINO. Jumuiya ya MT. ANDREA BOBOLA na MT. THERESIA WA AVILLA wajiandae.
  1. NDOA. (SOMA MATANGAZO YA “KWA MARA YA KWANZA TU”)
  2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Florence Philibert, baba  yake ni Philibert Semakula na mama yake ni Veneranda Kemilembe  anataka kufunga ndoa na Lucia Augustino, baba yake ni Augustino Mlinga na mama yake ni Agnes Faustine. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Alphonce Kankila, baba  yake ni Kankila Watelusi na mama yake ni Sesilia Mwanang’ombe  anataka kufunga ndoa na Ester Zabron, baba yake ni Zabron Kalilo na mama yake ni Grace Nicholaus. Wote wanasali katika parokia ya Nkuhungu, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Basil Ndetembea, baba  yake ni Joseph Kirango na mama yake ni Antonia Simon anataka kufunga ndoa na Suzana Ernest, baba yake ni Ernest Muhemeli na mama yake ni Mkatale Sigani. Wote wanasali katika parokia ya Kristu Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Deogratias Mutekanga, baba  yake ni Charles Sililo na mama yake ni Leticia John anataka kufunga ndoa na Rozaria Sikuku, baba yake ni Stanslaus Dakho na mama yake ni Anastazia Daati. Wote wanasali katika Parokia ya Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Sebastian Mathias, baba  yake ni Mathias Lubinsha na mama yake ni Eva Lameck anataka kufunga ndoa na Jackline Adelbert, baba yake ni Adelbert Kakoko na mama yake ni Sophia Charles. Wote wanasali katika parokia ya St. Joseph Cathedral“, Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Christopher Lejeto, baba  yake ni Richard Mazengo na mama yake ni Secilia Chidawali anataka kufunga ndoa na Juliana Mumbii, baba yake ni Mande Mumbii na mama yake ni Elizabeth Mumbii. Wote wanasali katika parokia ya Mt. Inyasi wa Loyola Kigango cha Peter Clavery, Jimbo Kuu la Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *