- Wazazi/walezi mnatangazi kuchukua fomu za ubatizo wa watoto wachanga katika ofisi ya Parokia. Ubatizo utafanyika tarehe 26/12/2024. Viongozi wa Jumuiya wajaze sehemu zao na kupiga mhuri wa Jumuiya.
- Waumini mnatangaziwa kuwa jumapili ijayo, tarehe 24/11/2024 tutahitimisha mavuno mwaka 2024. Hivyo, basi viongozi wa jumuiya mnaombwa kuwasilisha makusanyo ya jumuiya, majina, namba ya simu na kiasi alichotoa kila mwanajumuiya. Mwisho wa kuwasilisha ni Jumapili Tarehe 24/11/2024.
- Dominika ijayo siku ya kuhitimisha mavuno 2024 tutakuwa na mchango wa kuboresha kapu la baba. Waumini mnaombwa kuchangia chochote siku hiyo.
- Watu wazima ambao hawana Masakramenti mbalimbali pamoja na wa-kukiri Imani, mnaombwa kujiandikisha katika ofisi ya Makatekista.
- Tunashukuru Jumuiya ya MT. PETRO MTUME na MT. JEAN MARIA MUZEEY kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. CLARA WA ASISSI na (B) MT. AUGUSTINO. Jumuiya ya MT. ALPHONCE RODRIGUEZ, na MT. THERESIA WA AVILLA wajiandae.
- NDOA. (YASOMWE KATIKA MISA YA PILI TU)
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Martin Nderumo, wazazi wake ni Martin Massawe na Avelina Folonja anataka kufunga ndoa na Pauleta Thadei, wazazi wake ni Thadei Mushi na Bernadetha Lucas.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Michael Eckson, wazazi wake ni Eckson Mwampamba na Sitina Kasebele anataka kufunga ndoa na Beatrice William, wazazi wake ni William Msiwa na Veronica Mtungwa.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Esdory Richard, wazazi wake ni Richard Chacha na Selina Shirati anataka kufunga ndoa na Emelita Sharoni, wazazi wake ni Ramadhani Lemu na Flora Ernest.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Ainea Kadodo, wazazi wake ni Kadodo Mtango na Mary Mtango anataka kufunga ndoa na Josephine Angelo, wazazi wake ni Angelo Majula na Levina Chine.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Emmanuel Ally, wazazi wake ni Ally Khingengena na Jusline Kalinabene anataka kufunga ndoa na Lucy Louis, wazazi wake ni Louis Msensemya na Eledina Msoma.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Joshua Peter, wazazi wake ni John Lucumay na Anjelita Sanare anataka kufunga ndoa na Grace Bosco, wazazi wake ni Bosco Albini na Habiba Shabani.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Charles James, wazazi wake ni James Mushi na Hildegarda James anataka kufunga ndoa na Winner Emmanuel, wazazi wake ni Emmanuel Moshi na Secilia Lyamuya.
_________________________________________________________________________________________________
MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:
Parokiayakiwanjachandege.or.tz.
NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish
KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:
YOUTUBE: Kndege Parish
FACEBOOK: Parokia Ya Kndege
INSTAGRAM: Kndege_Parish
Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia