MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA 3 YA MAJILIO MWAKA ‘C’– 15/12/2024

  1. Waseminari wote waliofunga shule mnaombwa kukutana na Baba Paroko siku ya Jumanne kuanzia saa 3:00 asubuhi.
  • Novena ya Noel itaanza tarehe 16/12/2024 mara baada ya misa za asubuhi. Waamini wote mnakaribishwa kushiriki.
  • Semina ya wazazi na wasimamizi wa watoto wa ubatizo itafanyika Jumamosi tarehe 21/12/2024 katika ukumbi wa Mt. Inyasi kuanzia saa 3:00 asubuhi.
  • Kwaya ya Maria Mama wa Mungu itazindua Albam ya nyimbo za Maria inayoitwa “Tumshangilie Maria” tarehe 22/12/2024 hapa Kanisani katika misa tatu. Nyote mnakaribishwa.
  • Tamasha la ‘Christimas Carols’ litafanyika tarehe 22/12/2024 hapa Parokiani kuanzia saa 10:00 jioni. Nyote mnakaribishwa.
  • Kalenda mpya za Radio Maria kwa mwaka 2025 zinapatika nje kwa gharama ya Sh. 5,000/=
  • Viongozi wa jumuiya mnaombwa kuchukua bahasha za Krismasi kuanzia Jumanne katika ofisi ya Parokia.
  • Viongozi wa jumuiya mnatangaziwa kufanya sensa katika jumuiya zenu na kuziwasilisha katika ofisi ya Mratibu wa H/Walei.kabla ya tarehe 28/12/2024.
  • Viongozi wa jumuiya mnatangaziwa kuandaa Mpango kazi na kuuwasilisha kabla ya tarehe 28/12/204 kwa Mratibu wa H/Walei.
  1. Tarehe 28/12/2024 kutakuwa na sherehe ya watoto mashahidi, itakayofanyika Podium Mbwanga. Jumuiya zote mnaombwa kukamilisha mchango wa sherehe hiyo ambao ni sh. 100,000/= kwa kila jumuiya. Pia wazazi mnaombwa kuwanunulia watoto sare ya T-Sheti.
  1. Watu wazima wasio na masakramenti mbalimbali mnaombwa kujiandikisha katika ofisi ya makatekista. Mafundisho yataanza Ijumaa tarehe 3/1/2025.
  1. Tunashukuru Jumuiya ya MT. ANDREA BOBOLA  na  KRISTU MFALME  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. MICHAEL MALAIKA MKUU na (B) MT. PETER FEBAR.  Jumuiya ya WAT. JOACKIMU NA ANNA,  na MT. PAULO MIKI wajiandae.
  1. NDOA. (YASOMWE KATIKA MISA YA PILI TU)
  2. Kwa mara ya Pili: Ndg. Godfrey Laurence, wazazi wake ni Laurence Yusuph na Regina Gombati anataka kufunga ndoa na Gloria Samwel, wazazi wake ni Samwel Elifamili na Saraphina Mabura.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. John Augustino, wazazi wake ni Augustino Sirili na Oliva Kayoza anataka kufunga ndoa na Felista Xavery, wazazi wake ni Xavery Suday na Maria Joseph.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *