MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA 26 YA MWAKA ‘B’– 29/09/2024

  1. Jumamosi tarehe 5/10/2024 kutakuwa na kikao cha Wazazi/Walezi wa watoto wa Komnyo ya kwanza na Kipaimara kuanzia saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Inyasi.
  • Mkutano wa H/Walei uliopangwa kufanyika tarehe 5/10/2024 umesongezwa hadi tarehe 26/10/2024. Viongozi wa Jumuiya na Vyama vya kitume mnaombwa kuwasilisha Ajenda za kikao katika ofisi ya H/Walei kabla ya tarehe 19/10/2024.
  • Jumanne tarehe 01/10/2024 kutakuwa na Misa ya ufunguzi wa  mwezi wa Rozari Takatifu. Misa itatanguliwa na kusali Rozari kuanzia saa 10:00 alasiri na Misa itaanza saa 11:00 jioni. Kila jumuiya na chama cha kitumu imepangiwa siku ya kuongoza na kushiriki sala ya Rozari takatifu hapa parokiani. Viongozi wa jumuiya na vyama vya kitumu mnaombwa kupitia ubao wa matangazo kuona ratiba yenu ya kushiriki na kuongoza sala ya Rozari. Waumini wote mnaombwa kushiriki sala ya Rozari hapa parokiani kwa mwezi mzima.
  • Viongozi wa Jumuiya zifuatazo mnaombwa kuangalia ratiba ya misa za Jumuiya wiki hili katika ubao wa matangazo. MT. THERESIA WA MTOTO YESU,  MT.PETER FEBAR, MT. FRANCIS XAVERY, MT. JOHN DE BRITO, WAT. JOACKIM NA ANNA, MT. FRANCIS WA ASISSI, MOYO MT. WA YESU NA B.M.T.L. 
  • Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. YUDA THADEI, MT. NICHOLAUS OWEN, MT. ANDREA KAGWA, MT. ALPHONCE RODRIGUEZ, MT. KAROLI LWANGA, MT. ROBERT BELLARMINE. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. ANTONY WA PADUA, MT. PAULO MIKI,

MT. FRANCIS BORGIA, MT. PETER CLAVERY CHAMWINO, MT. AUGUSTINO, MT. GEMMA GALGAN.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.

  • Tunashukuru Jumuiya ya MT. STEPHANO  na  MT. KAROLI LWANGA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. MARIA GORETI na (B) MT YUDA THADEI.  Jumuiya ya MT. ANTONY WA PADUA,  na MT. NICHOLAUS OWEN wajiandae.
  • NDOA. (KATIKA MISA YA PILI NA YA TATU TU)
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Eusebi Cornelius, wazazi wake ni Cornelius Mashauri na Eulalia Maadabu anataka kufunga ndoa na Ludovica Martin, wazazi wake ni Martin Samare na Anjelina Vedastus.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Deogratius Lucas, wazazi wake ni Lucas Maunye na Yusta Pima anataka kufunga ndoa na Jesca Donard, wazazi wake ni Donard Boniphace na Witiness Anthony.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Stanslaus Joachim, wazazi wake ni Joachim John na Maria Swamee anataka kufunga ndoa na Rehema Said, wazazi wake ni Said Ikono na Hawa Hassan.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Elia Patsoni, wazazi wake ni Patsoni Kasyanju na Joyce Chale anataka kufunga ndoa na Frida Neston, wazazi wake ni Neston Songoro na Felista Zabron.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Alberto Maganga, wazazi wake ni Emmanuel Kapimpiti na Grace Mkamiti anataka kufunga ndoa na Makrata Shela, wazazi wake ni Richard Kasindi na Jane Thomas.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Alick Alexander, wazazi wake ni Alexander Kipinge na Junisia Kilimila anataka kufunga ndoa na Emiliana Mark, wazazi wake ni Mark Lasway na Floriana Donasian.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Adelhelm Adrehelm, wazazi wake ni Oddo Mlowe na Pelagia Mtenga anataka kufunga ndoa na Angela Anselem, wazazi wake ni Anselem Fredrick na Mary Frank.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Benedict Gaitan, wazazi wake ni Gaitan Lwimbo na Maria Mdemu anataka kufunga ndoa na Magreth Yona, wazazi wake ni Yona Songo na Evalina Songo.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Stanslaus Joachim, wazazi wake ni Joachim John  na mary swamee  anataka kufunga ndoa na Rehema Said  
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Tadei Zenus, wazazi wake ni Zenus Kwangu na Lightness Zenus anataka kufunga ndoa na Matrina John, wazazi wake ni Msafiri John  na Jeni Amos.

Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.

Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH.app inapatikana playstore.

Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH

Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE

Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *