MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA 2 YA MAJILIO MWAKA ‘C’– 08/12/2024

  1. Jumla kuu ya Fungu la kumi mwezi wa kumi na moja (11) tumekusanya kiasi cha Tsh. 18,303,500/=

Paroko anawashukuru waumini wote waliotoa zaka ya mwezi wa Kumi na moja. Mungu awabariki nyote.

  • Wazazi/walezi wa watoto wanaotarajia kubatiza tarehe 26/12/2024 mnatangaziwa kuwa mwisho wa kurudisha fomu ni alhamisi tarehe 12/12/2024.  Mahojiano yatafanyika siku ya ijumaa tarehe 13/12/2024 saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Inyasi.
  • Kwaya ya Maria mama wa Mungu itazindua Albam ya nyimbo za Maria inayoitwa “Tumshangilie Maria” uzinduzi utafanyika tarehe  22/12/2024 hapa Kanisani katika misa zote tatu. Nyote mnakaribishwa.
  • Fomu za kujiunga na kidato cha tano shule ya Secondary St. Peter Claver zinapatikana katika ofisi ya Parokia.
  • Mkutano wa H/Walei uliopangwa kufanyika tarehe 14/12/2024 umesongezwa hadi tarehe 18/01/2025. Viongozi wa Jumuiya na Vyama vya kitume mnaombwa kuwasilisha Ajenda za kikao katika ofisi ya H/Walei kabla ya tarehe 10/01/2025.
  • Taarifa na zawadi ya Mavuno kwa mwaka 2024 itatangazwa na kutolewa zawadi kwa jumuiya zilizo fanya vizuri Jumapili ya tarehe 15/12/2024 katika misa ya pili.
  • Tarehe 28/12/2024 kutakuwa na sherehe ya watoto mashahidi, itakayofanyika Podium Mbwanga. Jumuiya zote mnaombwa kukamilisha mchango wa sherehe hiyo ambao ni sh. 100,000/= kwa kila jumuiya. Pia wazazi mnaombwa kuwanunulia watoto sare ya T-Sheti.
  • Tunashukuru Jumuiya ya MT. ALPHONSUS RODRIGUEZ  na  MT. THERESIA WA AVILLA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MOYO MTAKATIFU WA YESU na (B) MT. BIKIRA MARIA NYOTA YA ASUBUHI.  Jumuiya ya MT. MICHAEL MALAIKA MKUU,  na MT. PETER FEBAR wajiandae.
  • NDOA. (YASOMWE KATIKA MISA YA PILI TU)
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Godfrey Laurence, wazazi wake ni Laurence Yusuph na Regina Gombati anataka kufunga ndoa na Gloria Samwel, wazazi wake ni Samwel Elifamili na Saraphina Mabura.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. John Augustino, wazazi wake ni Augustino Sirili na Oliva Kayoza anataka kufunga ndoa na Felista Xavery, wazazi wake ni Xavery Suday na Maria Joseph.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Johnson John, wazazi wake ni John Theodory na Eusebia Fidelis anataka kufunga ndoa na Julia Revocatus, wazazi wake ni Revocatus Muchunguzi na Anna Reverian.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *