MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA 17 YA MWAKA ‘B’– 28/07/2024

  1. Wajumbe wa H/Walei mnatangaziwa kuwa Mkutano utakuwa tarehe 10/8/24. Viongozi wa Jumuiya na Vyama vya Kitume mnaombwa kuwasilisha ajenda.  Mwisho wa kupokea ajenda ni leo.
  • Wazazi wa watoto waliopokea Kipaimara tarehe 14/7/24 pamoja na watu wazima walio pokea masakramenti mbalimbali mnaombwa kuchukua vyeti katika ofisi ya Parokia kuanzia Jumanne.
  • Watoto wote waliojiandikisha mafundisho ya Komnyo ya Kwanza, Kipaimara pamoja na watu wazima wa masakramenti mbalimbali mnatangaziwa kuwa mafundisho yataanza Ijumaa tarehe 2/8/24 saa 9:00 alasiri hapa Parokiani.
  • Viongozi wa WAWATA Parokia wanawakumbusha Viongozi wote wa WAWATA Jumuiya ambao Bado hawajawasilisha mchango wa kutengeneza Sanamu ya Bikira Maria Msaada wa Wakristo kuwasilisha michango hiyo ofisi ya WAWATA.
  • Jumuiya ya Mt. Yuda Thadei inawatangazia waamini wote kuwa kuanzia 01/8/2024 wataanza kukodisha vyombo vya Muziki katika Sherehe mbalimbali. Waamini wanaparokia watakuwa na bei yao maalumu. Kwa maelezo zaidi pitia katika ubao wa matangazo.
  • M/Kiti wa Uwaka K/Ndege kwa niaba ya Kamati Tendaji anawaalika Wana-Uwaka wote kuhudhuria Mkutano Jumamosi tarehe 3/8/2024 saa 4:00 asubuhi.  Mnaombwa kuleta ajenda kwa Katibu ofisini.
  • Jumamosi tarehe 03/08/2024 saa 3:00 asubuhi Kutakuwa na mahojiano ya wazazi wa watoto watakao batizwa tarehe 17/8/2024.
  • Fomu za kujiunga na Kidato cha kwanza Shule ya Olale iliyopo Jimbo la Moshi zinapatikana hapa Parokiani.
  • Kesho Tarehe 29/07/2024 mpaka tarehe 3/08/2024 kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 1:00 jioni kutakuwa na mafunzo ya usalama barabarani hapa parokiani. Mafunzo haya ni bure kwa watu wote ila kwa wasio na vyeti watachangia gharama nafuu na watakao kuhitaji kujifunza gari kwa vitendo zitakuwepo. Kwa mawasiliano zaidi piga 0756 299 929.
  1. Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. GABRIEL MALAIKA MKUU, MT. ANDREA BOBOLA, WAT. JOACKIMU NA ANNA, MT. URSULA, MT. THERESIA WA MTOTO YESU, MT. PHILIPO EVANS. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. FRANCIS JEROME, MT. AGATHA, MT. STANSLAUS KOSTIKA, KRISTU MFALME, MT. JEAN MARIA MUZEEY, MOYO MTAKATIFU WA YESU.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
  1. Tunashukuru Jumuiya ya WAT. JOACKIM NA ANNA   na  MT. FRANCIS BORGIA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. YOHANE PAULO WA II na (B) MT JOSEPHINE BAKITA.  Jumuiya ya MT. ALOYCE GONZAGA,  na MT. JOHN DE BRITO wajiandae.
  1. NDOA.
  2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Mathei Kalisti, wazazi wake ni Kalisti Mwibu na Petronila Zakaria anataka kufunga ndoa na Happyness Gasto, wazazi wake ni Gasto Tito na Leah Zabron.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Kelvin Ladislaus, wazazi wake ni Ladislaus Kilonda na Christina Ngajiro anataka kufunga ndoa na Mariam Gerson, wazazi wake ni Gerson Mangula na Sevelina Funguo.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Albert Wagili, wazazi wake ni Joseph Sabeli na Josephina Ngiliule anataka kufunga ndoa na Rose Mbuva, wazazi wake ni Leons Safari na Everilda Buli.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Andrew Julius, wazazi wake ni Julius Mselemu na Salvatorian  Katunzi anataka kufunga ndoa na Mary Exaud, wazazi wake ni Axaud Mbise na Apaikunda Matayo.

Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.

Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH.  app inapatikana playstore. Waumini Mnaombwa kujisajili kijumuiya kwa app.  

Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH

Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE   

Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *