MATANGAZO, Uncategorized

MATANGAZO YA DOMINICA YA 10 YA MWAKA ‘B’– 09/06/2024

  1. Jumla kuu ya Fungu la kumi mwezi wa Tano tumekusanya kiasi cha Tsh. 16,944,550/=

*Tunawashukuru wote waliotoa kwa moyo wa ukarimu wakiwemo waliotoa kupitia mfumo wa sadaka dijital*

  • Waumini mnakumbuswa kuchukua bahasha za fungu la kumi kila Jumapili ya kwanza ya mwezi na  mnapozirudisha tumbukizeni kwenye masanduku ya sadaka.                                       
  • Fomu za kujiunga na kidato cha kwanza shule ya Secondary ya St. Peter  Claver Ihumwa zinapatikana katika Ofisi ya Parokia.
  • Shule ya Msingi na Chekechea Almes Dodoma wanawatangazia nafasi za masomo kwa Mwaka 2024/2025.  Pia wanatoa huduma kwa watoto wenye uhitaji maalumu, kwa maelezo zaidi pita katika ubao wa matangazo.
  • Uongozi wa Wawata Parokia wanawatangazia Vijana wote kuwa kutakuwa na Semina siku ya Ijumaa tarehe 14/6/2024 kuanzia saa 9:00 alasiri na siku ya Jumamosi tarehe 15/6/2024 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:30 mchana. Wazazi mnaombwa kuhamasisha vijana waweze kushiriki katika semina hizo.
  • Uongozi wa Vijana Parokia wanawatangazia vijana wote kuwa jumapili tarehe 16/6/2024 watakuwa na ziara ya Uinjilishaji pamoja na Michezo katika Parokia ya Kizota. Kila mshiriki atapaswa kuchangia Tsh. 3,000/= kwa ajili ya chakula.  Michango iwasilishwe katika ofisi ya vijana na Mwisho wa mchango ni tarehe 15/6/2024 usafiri utatoka Parokiani.
  • Tarehe 7/7/2024 kutakuwa na sherehe ya somo wa Parokia. Jumuiya zinatakiwa kuandaa chakula kwa siku hiyo. Sherehe itatanguliwa na Semina itakayofanyika tarehe 30/06/2024.
  • Tarehe 29/06/2024 kutakuwa na Mkutano Maalum wa H/Walei. Wajumbe wote wa Kamati Tendaji za jumuiya pamoja na wenyeviti wa Vyama vya kitume ngazi ya Parokia mnaombwa kushiriki.
  • Uongozi wa Uwaka Parokia wanawatangazia Wanaume wote kuwa kutakuwa na Mkutano wa Dharura tarehe 15/6/2024 siku ya Jumamosi saa 3:30 asubuhi.
  1. Magazeti ya kiongozi na Enendeni yanapatikana hapo nje.
  1. Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. JOSEPHINE BAKITA, MT. YOHANE PAULO II, MT. MAXIMILIAN KOLBE, MT. YOHANE WA MSALABA, MT. CLARA WA ASISSI, MT. FRANCIS WA ASISSI. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. GABRIEL MALAIKA MKUU, MT. ANDREA BOBOLA, WAT. JOACKIMU NA ANNA, MT. URSULA, MT. THERESIA WA MTOTO YESU, MT. PHILIP EVANS.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
  1. Tunashukuru Jumuiya ya MT. PHILIP EVANS   na  SHIRIKA LA MOYO MTAKATIFU WA YESU  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. KATARINA WA SIENA na (B) MT. URSULA.  Jumuiya ya MT. ANTONY DANIEL,   na MT. MARIA GORETH wajiandae.
  1. NDOA. (SOMA MATANGAZO YA “KWA MARA YA KWANZA TU”)
  2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Gerald Joseph, baba  yake ni Joseph Gondo na mama yake ni Sarafina Thomas anataka kufunga ndoa na Claudia Laurent, baba yake ni Laurent Bugaya na mama yake ni Irene Johnface. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Amos Sengule, baba  yake ni Sengule Gangila na mama yake ni Magen Ludaba anataka kufunga ndoa na Elizabeth Paskali, baba yake ni Paskali Kasanga na mama yake ni Dina Balaliga. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Emmanuel Mng’ong’o, baba  yake ni Wilbert Mng’ong’o na mama yake ni Desteria Nyoni anataka kufunga ndoa na Magreth Meshack, baba yake ni Meshack Chalo na mama yake ni Coleth Kivike. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Cosmas Gidion, baba  yake ni Gidion Ambrose na mama yake ni Devidika Shaibu anataka kufunga ndoa na Elizabeth Evarist, baba yake ni Evarist Adabu na mama yake ni Maria Sakina. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Daudi Jeremia, baba  yake ni Jeremia Peremena na mama yake ni Elizabeth Mbogo anataka kufunga ndoa na Imelda Gidion, baba yake ni Gidion Mng’ong’o  na mama yake ni Frida Mng’ong’o. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Boniface Emmanuel, baba  yake ni Juma Hassan na mama yake ni Dorothea Mwisi anataka kufunga ndoa na Maria Mtipa, baba yake ni John Hokololo na mama yake ni Agnes Milanzi. Wote wanasali katika parokia ya Kange – Jimbo Katoliki la Tanga.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. John Malima, baba  yake ni Jeremia Malima na mama yake ni Gemma Manzala anataka kufunga ndoa na Bertha Charles, baba yake ni Charles Kabenga na mama yake ni Anna Mbalamwezi. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Gregory Severin, baba  yake ni Severin Kissato  na mama yake ni Valeriana Kuwingwa anataka kufunga ndoa na Angela Eugenus, baba yake ni Eugenus Mlula na mama yake ni Mariana Mlula. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  1. Kwa mara ya Pili: Ndg. Daudi Gaudensi, baba  yake ni Gaudensi Mlelema  na mama yake ni Albertina Magayu anataka kufunga ndoa na Fatuma Hamisi, baba yake ni Hamisi Iddi na mama yake ni Furaha Hamisi. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili Ndg Hilary Mapunda baba  yake ni Hilary Klodwig na mama yake ni Chiku Athumani anataka kufunga ndoa na Bernadetha Kiswaga baba yake ni David Raphael na mama yake ni  Grace Magolyo.  Wote wanasali katika parokia ya Iyumbu-Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Peter Simon, baba  yake ni Simon Chuwa  na mama yake ni Yasinta Epimark anataka kufunga ndoa na Ester John, baba yake ni John Matias na mama yake ni Juliana John. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Michael  Emmanuel, baba  yake ni Emmanuel Michael  na mama yake ni Pasquina John anataka kufunga ndoa na Taji Jobu, baba yake ni Jobu Fundi na mama yake ni Lucy Fonga. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Jackson Sibora, baba  yake ni Joseph Sibo na mama yake ni Penina Songa  anataka kufunga ndoa na Joyce Hugo, baba yake ni Hugo  na mama yake ni Magreth Mapunda. Wote wanasali katika parokia ya Ifunda – Jimbo Katoliki la Iringa.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Barthalomeo Mkalawa, baba  yake ni Erenesti Mkalawa na mama yake ni Maliselina Lukwawila anataka kufunga ndoa na Beatrice Elisante, baba yake ni Elisante Lyatuu na mama yake ni Egla Harold. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Godfrey Frumens, baba  yake ni Frumens Oswin na mama yake ni Zabibu Abuu anataka kufunga ndoa na Irene Costantin, baba yake ni Costantin Selestin na mama yake ni Caroline Ally. Wote wanasali katika parokia ya Mt. Polycarp– Misugusugu Pwani – Jimbo Kuu Katoliki la Dar-es-Salaam.
  • Kwa mara ya Tatu, Ndg Gaspar Gomora baba yake ni Gomora na mama yake ni Renada Kimulela anataka kufunga ndoa na Alida baba yake ni Innocent na mama yake ni Adventina Martine. Wote wanasali katika parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani, Kasumo, Jimbo la Kigoma.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Emmanuel Mchemwa, baba  yake ni Martin Luka na mama yake ni Margarita Njuu anataka kufunga ndoa na Balbina Victor, baba yake ni Victor Joseph na mama yake ni Luisa Palakata. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege– Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Oscar Kalinga, baba  yake ni Cassian Kalinga na mama yake ni Fatu Koga anataka kufunga ndoa na Margreth Haule, baba yake ni Walter Ngunguru na mama yake ni Maria Haule. Wote wanasali katika parokia ya Mafinga – Jimbo Katoliki la Iringa.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:parokiayakiwanjachandege.or.tz. PIA TEMBELEA YOUTUBE YA PAROKIA KWA MATUKIO MBALIMBALI YA PAROKIA.    

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *