MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA 1 YA MAJILIO MWAKA ‘C’– 01/12/2024

  1. Kutakuwa na uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi za viongozi zilizo achwa wazi. Uchaguzi utafanyika Jumamosi tarehe 7/12/2024.  Viongozi wa jumuiya na vyama vya kitume mnaombwa kuwasilisha taarifa za nafasi zilizo wazi kwenye ofisi ya H/Walei. Mwisho wa kupokea taarifa hizo ni tarehe 3/12/2024.
  • Mkutano wa halmashauri Walei parokia utafanyika tarehe 14.12.2024 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Inyasi. Viongozi wa jumuiya na vyama vya kitume mnaombwa kuwasilisha agenda katika ofisi ya halmashauri Walei kabla ya tarehe 10.12.2024.
  • Tarehe 28/12/2024 kutakuwa na sherehe ya watoto mashahidi, itakayofanyika Podium Mbwanga. Jumuiya zote mnaombwa kukamilisha mchango wa sherehe hiyo ambao ni sh. 100,000/= kwa kila jumuiya. Pia wazazi mnaombwa kuwanunulia watoto sare ya T-Sheti.
  • Tunashukuru Jumuiya ya MT. CLARA WA ASISSI  na  MT. AUGUSTINO  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. ANDREA BOBOLA na (B) KRISTU MFALME.  Jumuiya ya MOYO MTAKATIFU WA YESU,  na MT. BIKIRA MARIA NYOTA YA ASUBUHI wajiandae.
  • NDOA. (YASOMWE KATIKA MISA YA PILI TU)
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. John Augustino, wazazi wake ni Augustino Sirili na Oliva Kayoza anataka kufunga ndoa na Felista Xavery, wazazi wake ni Xavery Suday na Maria Joseph.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Johnson John, wazazi wake ni John Theodory na Eusebia Fidelis anataka kufunga ndoa na Julia Revocatus, wazazi wake ni Revocatus Muchunguzi na Anna Reverian.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Martin Nderumo, wazazi wake ni Martin Massawe na Avelina Folonja anataka kufunga ndoa na Pauleta Thadei, wazazi wake ni Thadei Mushi na Bernadetha Lucas.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *