MATANGAZO

DOMINIKA YA 21 MWAKA B WA KANISA

Tarehe 28/08/24 siku ya Jumatano Padre atafanya ziara za kichungaji katika jumuiya ya MT. DEVID LEWIS na tarehe 30/08/24 siku ya Ijumaa katika Jumuiya ya MT. JOHN DE BRITO kuanzia saa 8:30 alasiri. Wiki ijayo wajiandae Jumuiya za MT. FRANCIS EXAVERY Na MT. ANTONY DANIEL.

    • Waamini wanawake wenye changamoto ya kufika katika vyoo vilivyoko mwisho wa parking wanaombwa kutumia vyoo vilivyoko katika ukumbi wa Mt. Inyasi, karibu na vyoo vya walemavu. Vivyo hivyo, waamini wanaume wenye changamoto hiyo, wanaombwa kutumia vyoo vilivyoko karibu na konteina.
    • Wazazi wa watoto walio batizwa tarehe 17/08/2024 mnaombwa kuchukuwa vyeti vyenu katika ofisi ya Parokia kuanzia jumanne.
    • Ratiba ya Semina ya Mavuno juyiyani inapatikana katika ubao wa Matangazo. Pia Mpangokazi wa mafundisho ya Ndoa unapatikana katika ubao wa Matangazo.
    • Viongozi wa jumuiya mnaombwa kuchukua bahasha za Mavuno kuanzia jumanne katika ofisi ya Parokia.
    • Jumuiya ambazo hazijarejesha Fomu za Sensa ya waamini mnaombwa kurejesha Parokiani.
    • Uongozi wa vijana unawajulisha kuwa watakuwa na Hija ya vijana Jimbo kuu la Mwanza kituo cha Maria Rita, pamoja na ziara katika Parokia ya Nyakahoja kuanzia tarehe 13/09/2024 hadi 16/09/2024. Gharama kwa kila mshiriki ni 120,000/= mwisho wa mchango ni tarehe 1/09/2024.         
    • Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. PAULO MIKI, MT. FRANCIS BORGIA, MT. PETER CLAVERY, MT. AUGUSTINO, MT. GEMMA GALGAN, MT. MONICA.  Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. ANTONY DANIEL, MT. DAVID LEWIS, MT. JOSEPHINE BAKITA, MT. YOHANE PAULO WA II, MT. MAXIMILIAN KOLBE, MT. YOHANE WA MSALABA.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
    • Tunashukuru Jumuiya ya MT. PIO  na  MT. AGATHA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. ROBERT BELLARMINE na (B) MT KIZITO.  Jumuiya ya MT. STANSLAUS KOSTIKA,  na B.M.T.L wajiandae.
    1. NDOA.
    2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Melkiori Majani, wazazi wake ni Severini Jumapili na Evangelista Khoaa anataka kufunga ndoa na Ester Bernard, wazazi wake ni Bernard Stephen na Anna Saulo.
    • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Joseph Sefu, wazazi wake ni Ally Sefu na Christer Paulo anataka kufunga ndoa na Anastazia Richard, wazazi wake ni Richard Mankaba na Merana Augustino.
    • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Dickson Sanga, wazazi wake ni Jimson Sanga na Bernadetha Nihume anataka kufunga ndoa na Magdalena Kibodya, wazazi wake ni Erasto Kibodya na Rehema Mgao.
    • Kwa mara ya Pili: Ndg. Chrispo Nicholaus, wazazi wake ni Nicholaus Lwila na Betseba Lwila anataka kufunga ndoa na Dorothea Deodatus, wazazi wake ni Deodatus Mlokozi na Agnes Kokusimbisa.

    Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.

    Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH.  app inapatikana playstore.

    Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH

    Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE   

    Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia

    Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *