MATANGAZO YA DOMINICA YA 20 YA MWAKA ‘B’– 18/08/2024
- Jumapili tarehe 25/08/2024 ni uzinduzi wa Mavuno kwa Mwaka 2024, Viongozi wa jumuiya mnaombwa kupitia ubao wa Matangazo kuangalia ratiba ya semina ya Mavuno kwenye jumuiya zenu.
- Kuanzia jumapili ijayo tarehe 25/08/2024 Misa ya Kiingereza itakuwa inaanza saa 4:00 asubuhi.
- Shule za Trust St. Patrick iliyopo Arusha zinawatangazia nafasi za kujiunga na shule ya Msingi hadi Secondary. Kwa maelezo zaidi kuna vipeperushi getini.
- Mafundisho ya ndoa yatakuwa tarehe 23, 24 na 25/08 /2024. Wanaotarajia kufunga ndoa wajiandikishe.
- Kwaya ya Ledochowska inawatangazia waamini wote kuwa wageni kutoka Rwanda watafika hapa Parokiani tarehe 23/08/2024. Hivyo wanawaomba muwaunge mkono kwa kuwapokea na kununua tiketi ambazo zinauzwa kwa gharama ya Tsh. 20,000/= kwa watu wazima, watoto 10,000/= na VIP 100,000 tu.
- Waamini wanawake wenye changamoto ya kufika katika vyoo vilivyoko mwisho wa parking wanaombwa kutumia vyoo vilivyoko katika ukumbi wa Mt. Inyasi, karibu na vyoo vya walemavu. Vivyo hivyo, waamini wanaume wenye changamoto hiyo, wanaombwa kutumia vyoo vilivyoko karibu na konteina.
- Uongozi wa vijana unawajulisha kuwa watakuwa na Hija ya vijana Jimbo kuu la Mwanza kituo cha Maria Rita, pamoja na ziara katika Parokia ya Nyakahoja kuanzia tarehe 13/09/2024 hadi 16/09/2024. Gharama kwa kila mshiriki ni 120,000/= mwisho wa mchango ni tarehe 1/09/2024.
- Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. NICHOLAUS OWEN, MT. ANDREA KAGWA, MT. ALPHONSUS RODRIGUEZ, MT. KAROLI LWANGA, MT. ROBERT BELLARMINE, MT. ANTONY WA PADUA. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. PAULO MIKI, MT. FRANCIS BORGIA, MT. PETER CLAVERY, MT. AUGUSTINO, MT. GEMMA GALGAN, MT. MONICA.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
- Tunashukuru Jumuiya ya MT. ALOYCE GONZAGA na MT. JOHN DE BRITO kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. MAGRETH MARIA ALACOQUE na (B) MT SIMONI ZELOTE. Jumuiya ya MT. ROBERT BELLAMINE, na MT. KIZITO wajiandae.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Robert Paul, wazazi wake ni Paul Elias na Ester Issa anataka kufunga ndoa na Victoria Francis, wazazi wake ni Francis Benezeth na Sesilia Alphonce.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Kedmon Mnyamagola, wazazi wake ni Leonard Mnyamagola na Magdalena Mnyamagola anataka kufunga ndoa na Rehema Wilson, wazazi wake ni Wilson Chilamba na Siflasi Mnyiri.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Yoshua Emmanuel, wazazi wake ni Emmanuel Youze na Merina Richard anataka kufunga ndoa na Merina David, wazazi wake ni Michael David na Narowil Sabaya.
Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.
Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH. app inapatikana playstore.
Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH
Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE
Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia