MATANGAZO, Uncategorized

MATANGAZO YA DOMINICA YA MWILI NA DAMU YA BWANA WETU YESU KIRSTO MWAKA ‘B’– 02/06/2024

  1. Waumini mnakumbuswa kurudisha bahasha za fungu la Kumi na kuzitumbukiza kwenye masanduku ya sadaka.
  • Ratiba ya misa za Jumuiyani mwezi wa 6 inapatikana katika ubao wa Matangazo na katika Tovuti ya parokia. Viongozi mnaombwa kusoma na kuwasiliana na paroko iwapo tarehe mliyopangiwa ni tofauti na mipango ya jumuiya.
  • Jumapili ya ijayo tarehe 9/6/2024, tutamshika mkono Sister Deodata kumpongeza kwa kuweka nadhiri za daima. Waumini mnaombwa kumpa chochote ili kumshukuru Mungu kwa wito na utume wake hapa parokiani.   
  • Waumini mnatangaziwa kuwa kuanzia tarehe 13 mpaka 15 mwezi huu wa 6, kutakuwa na kongamano la Biblia Takatifu katika parokia ya Nala. Ratibu nzima inapatikana katika ubao wa matangazo.
  • Fomu za kujiunga na Seminary za Consolata Mafinga na Bihawana zinapatikana katika Ofisi ya Parokia.
  • Tarehe 7/7/2024 kutakuwa na sherehe ya somo wa Parokia.  Jumuiya zinatakiwa kuandaa chakula kwa siku hiyo.  Sherehe itatanguliwa na Semina itakayofanyika tarehe 30/06/2024.
  • Wanandoa waliotimiza au wanaotarajia kutimiza miaka 25, 50 ya ndoa mwaka huu wajiandikishe katika ofisi ya parokia kabla ya tarehe 15 Juni.
  • Viongozi wa Jumuiya na Kanda ambazo zina nafasi wazi za Viongozi, zinajulishwa kuwa uchaguzi wa viongozi utafanyika tarehe 8/6/2024.  Taarifa kuhusu jumuiya na Kanda zinazohitaji kufanya uchaguzi ziwasilishwe Ofisi ya Parokia kabla ya tarehe 5/6/2024.
  • Tarehe 22/6/2024 kutakuwa na Mkutano maalum wa H/Walei utakaofanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Inyasi. Mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kujadili na kupitisha kanuni za uendeshaji wa Parokia. Viongozi wote wa Jumuiya na wenyeviti wa vyama vya kitume ngazi ya Parokia mnaombwa kushiriki bila kukosa.
  1. Magazeti ya kiongozi na Enendeni yanapatikana hapo nje.
  1. Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. PETER CLAVER CHAMWINO, MT. AUGUSTINO, MT. GEMMA GALGAN, MT. MONICA, MT. ANTONY DANIEL, MT. DAVID LEWIS. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. JOSEPHINE BAKITA, MT. YOHANE PAULO II, MT. MAXIMILIAN KOLBE, MT. YOHANE WA MSALABA, MT. CLARA WA ASISSI, MT. FRANCIS WA ASISSI.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
  1. Tunashukuru Jumuiya ya KRISTU MFALME   na  KARISMATIKI  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. GEMMA GALGAN na (B) MT. BIKIRA MARIA NYOTA YA ASUBUHI.  Jumuiya ya MT. KATARINA WA SIENA,   na MT. URSULA wajiandae.
  1. NDOA. (SOMA MATANGAZO YA “KWA MARA YA KWANZA TU”)
  2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. John Malima, baba  yake ni Jeremia Malima na mama yake ni Gemma Manzala anataka kufunga ndoa na Bertha Charles, baba yake ni Charles Kabenga na mama yake ni Anna Mbalamwezi. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Gregory Severin, baba  yake ni Severin Kissato  na mama yake ni Valeriana Kuwingwa anataka kufunga ndoa na Angela Eugenus, baba yake ni Eugenus Mlula na mama yake ni Mariana Mlula. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Daudi Gaudensi, baba  yake ni Gaudensi Mlelema  na mama yake ni Albertina Magayu anataka kufunga ndoa na Fatuma Hamisi, baba yake ni Hamisi Iddi na mama yake ni Furaha Hamisi. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza Ndg Hilary Mapunda baba  yake ni Hilary Klodwig na mama yake ni Chiku Athumani anataka kufunga ndoa na Bernadetha Kiswaga baba yake ni David Raphael na mama yake ni  Grace Magolyo.  Wote wanasali katika parokia ya Iyumbu-Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Peter Simon, baba  yake ni Simon Chuwa  na mama yake ni Yasinta Epimark anataka kufunga ndoa na Ester John, baba yake ni John Matias na mama yake ni Juliana John. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Michael  Emmanuel, baba  yake ni Emmanuel Michael  na mama yake ni Pasquina John anataka kufunga ndoa na Taji Jobu, baba yake ni Jobu Fundi na mama yake ni Lucy Fonga. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Jackson Sibora, baba  yake ni Joseph Sibo na mama yake ni Penina Songa  anataka kufunga ndoa na Joyce Hugo, baba yake ni Hugo  na mama yake ni Magreth Mapunda. Wote wanasali katika parokia ya Ifunda – Jimbo Katoliki la Iringa.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Barthalomeo Mkalawa, baba  yake ni Erenesti Mkalawa na mama yake ni Maliselina Lukwawila anataka kufunga ndoa na Beatrice Elisante, baba yake ni Elisante Lyatuu na mama yake ni Egla Harold. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege – Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  1. Kwa mara ya Pili: Ndg. Godfrey Frumens, baba  yake ni Frumens Oswin na mama yake ni Zabibu Abuu anataka kufunga ndoa na Irene Costantin , baba yake ni Costantin Selestin na mama yake ni Caroline Ally. Wote wanasali katika parokia ya Mt. Polycarp– Misugusugu Pwani – Jimbo Kuu Katoliki la Dar-es-Salaam.
  • Kwa mara ya Pili, Ndg Gaspar Gomora baba yake ni Gomora na mama yake ni Renada Kimulela anataka kufunga ndoa na Alida baba yake ni Innocent na mama yake ni Adventina Martine. Wote wanasali katika parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani, Kasumo, Jimbo la Kigoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Emmanuel Mchemwa, baba  yake ni Martin Luka na mama yake ni Margarita Njuu anataka kufunga ndoa na Balbina Victor, baba yake ni Victor Joseph na mama yake ni Luisa Palakata. Wote wanasali katika parokia ya K/Ndege– Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Oscar Kalinga, baba  yake ni Cassian Kalinga na mama yake ni Fatu Koga anataka kufunga ndoa na Margreth Haule, baba yake ni Walter Ngunguru na mama yake ni Maria Haule. Wote wanasali katika parokia ya Mafinga – Jimbo Katoliki la Iringa.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Kelvin Moris, baba  yake ni Moris Garigo na mama yake ni Flora Aloyo anataka kufunga ndoa na Fauster Alphonce, baba yake ni Alphonce Nyiridandi na mama yake ni Flavia Kazoba. Wote wanasali katika parokia ya Kinyerezi, Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Lucas Magacha, baba  yake ni Stephano Kikube na mama yake ni Annastazia Bhoke anataka kufunga ndoa na Lightness Emmanuel, baba yake ni Emmanuel Machiya na mama yake ni Clara Rashidi. Wote wanasali katika parokia ya B.M.M. wa Mwokozi Sinza, Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Michael Chota, baba  yake ni Jackson Machela na mama yake ni Estelina Kisenga anataka kufunga ndoa na Happy Kenan, baba yake ni Kenan Nkinela na mama yake ni Agnes Chanai. Wote wanasali katika parokia ya Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu la Dodoma.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:parokiayakiwanjachandege.or.tz  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *