MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 2 PASAKA MWAKA ‘C’– 27/04/2025

  1. Tarehe 1/5/2025 kutakuwa na uzinduzi wa mwezi wa Mama Maria. Maandamano ya sala ya rozari yataanza saa 10:00 jioni na baadae Misa saa 11:00 jioni. Waamini mnahimizwa kushiriki.
  • Kila Ijumaa ya mwezi wa Maria, Rozari itakuwa inaanza saa 10:30 jioni na kufuatiwa na semina saa 11:00 joni. Waamini wote mnaombwa kufika bila kukosa.
  • Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kurejesha mchango wa sherehe ya upadrisho kama mlivyopangiwa; na waamini waliochukua kadi na fomu za mchango huo mnaombwa pia kurejesha mchango huo.  Tunawashukuru Jumuiya ya Mt. Andrea Kagwa kwa kumaliza mchango wao kwa wakati, pia Jumuiya za Mt. Aloyce Gonzaga, Mt. Robert Bellarmine, na Mt. Maria Goreth kwa kupunguza michango wao.
  • T-Sheti za wakubwa na watoto, vikoi, na vikombe vya Upadrisho na Sherehe ya Parokia vinapatikana nje katika duka la VIWATA.
  • Viongozi wa Jumuiya mnakumbushwa kutoa mchango wa Kongamano la Utoto Mt. Kanda (DOSIKO). Kila jumuiya itoe kiasi cha 130,000/= kwa kila mshiriki kadri ya barua ilivyoelekeza.  Mwisho wa kuwasilisha michango hiyo ni tarehe 15/05/2025.
  • Chama cha Mt. Rita wa Kashia Jimbo la Dodoma kimeandaa Hija kuelekea Kiabakari Musoma na Kituo cha Mlima wa Sala Mwanza. Gharama za safari ni Sh. 250,000/= Kwa maelezo zaidi wasiliana na uongozi wa Mt. Rita wa Kashia Parokia.
  • Mafundisho ya wakatekumeni na masakramenti mbalimbali kwa watu wazima, pamoja na wale wa kukiri Imani yataanza Ijumaa tarehe 2/5/2025  hapa Parokia.
  • Tunawashukuru Jumuiya ya MT. PETRO MTUME  na  MT. MAXIMILIAN KOLBE  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada.  Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. CLARA WA ASISSI na (B) MT. MONICA.  Jumuiya ya MT. ALPHONSUS RODRIGUEZ  na MT. AUGUSTINO, wajiandae.
  • NDOA.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Albert Hilu, wazazi wake ni Antony Nginwa na Monica Makeja anataka kufunga ndoa na Agatha Nganga, wazazi wake ni Celestine Nganga na Zena Mbaraka.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Godfrey Medard, wazazi wake ni Medard Philbert na Flora Buyogere anataka kufunga ndoa na Subira Fred, wazazi wake ni Fred Mwasambili na Agatha Adolph.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Onesphory Africano, wazazi wake ni Africano Onesphory na Anna January anataka kufunga ndoa na Brenda Elia, wazazi wake ni Elia Daniel na Aurelia John.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *