MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 3 YA KWARESIMA MWAKA ‘C’– 23/03/2025

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 3 YA KWARESIMA MWAKA ‘C’– 23/03/2025

  1. Tarehe 28/03/2025 siku ya Ijumaa, Njia ya Msalaba wataongoza KANDA yaSAMARIA na YUDEA na Kwaya ya B.M.T.L, pamoja na kutoa vipaji.KANDA ya GETHSEMAN na Kwaya ya MT. GEMA GALGAN wajiandae.
  • Wazazi/walezi mnatangaziwa kuchukua fomu za Ubatizo wa watoto wachanga katika Ofisi ya Parokia. Ubatizo utafanyika tarehe 21/04/2025 Jumatatu ya Pasaka. Viongozi wa Jumuiya wajaze sehemu zao na kupiga mhuri wa Jumuiya fomu hizo.
  • Kanisa dogo la kuabudia litafunguliwa Jumanne ijayo.
  • Parokia ya K/Ndege imeandaa sala, semina, na mafungo kwa makundi mbalimbali. Waamini mnahimizwa kushiriki kadiri ya kundi na kwa tarehe husika. Tarehe 5 – 6/4/2025 tutaanza na Wagonjwa na Wahudumu wa Afya. Semina itaanza saa 9:00 alasiri. Ratiba nzima inapatikana katika ubao wa matangazo.
  • Jumapili ijayo kutakuwa na uhamasishaji juu ya utoaji wa zaka na michango mingine katika misa zote.
  • Jumapili ijayo kutakuwa na semina maalum ya Kwaresima ya watoto itakayoanza saa 03:00-05:00 asubuhi na itakayoongozwa na wanovisi Wajesuiti katika Ukumbi wa Mt Inyasi.  Wazazi na walezi mnaombwa kuwaleta watoto mapema ili waweze kuhudhuria semina hiyo.
  • Utume wa Karismatiki Katoliki Dekania ya Paulo wa Msalaba wameandaa semina inayohusu toba na msamaha itakayofanyika Parokiani K/Ndege kuanzia tarehe 28 – 30/3/2025 kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 12:00 jioni. Waamini wote mnakaribishwa.
  • Tarehe 05/04/2025 kutakuwa na mkutano wa H/Walei katika ukumbi wa Inyasi. Viongozi wa Jumuiya na vyama vya kitume mnaombwa kuwasilisha ajenda za mkutano huo katika ofisi ya H/Walei kabla ya tarehe 1/04/2025.
  • Jumanne tarehe 25/03/2025 tutatembelewa na Radio Maria kwenye Misa za asubuhi. Watarusha hewani sala ya Malaika wa Bwana pamoja na masifu ya asubuhi vikifuatiwa na Misa takatifu. Waamini pamoja na vyama vya kitume mnaalikwa kushiriki na wana Radio Maria.
  1. Alhamisi tarehe 27/03/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya YERIKO. Alhamisi  ijayo tarehe 03/04/2025 wajiandae Kanda ya YERUSALEMU.Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
  1. Kitabu kinachotoa mafunzo ya afya ya akili na magonjwa ya akili kama vile msongo wa mawazo, sonona, na magonjwa mengine yanayo husu afya ya akili kilicho andikwa na Ndugu Peter Njau kinapatikana getini kwa gharama ya Tsh. 6,000/=
  1. Tunawashukuru Jumuiya ya MT. MARIA GORETH  na  MT. ANDREA KAGWA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. FRANCIS XAVERY na (B) MT. NICHOLAUS OWEN Jumuiya ya MT. PETER CLAVERY  na MT. BERNADETHA wajiandae.
  1. NDOA.
  2. Kwa mara ya Tatu: Ndg. Denis Amani, wazazi wake ni Wilhard Joseph na Philotea Vumilia anataka kufunga ndoa na Nice Jackson, wazazi wake ni Jackson Massawe na Evaristina Leoni.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:YOUTUBE: Knd

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *