Uncategorized

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 8 YA MWAKA ‘C’– 02/03/2025

  1. Viongozi wa Jumuiya mnaombwa kuchukua bahasha za Pasaka katika Ofisi ya Parokia.
  • Waamini wote wenye matawi majumbani mnaombwa kuyaleta Kanisani kwa ajili ya maandalizi ya Jumatano ya Majivu. Matawi yaletwe siku ya Jumatatu na Jumanne tu. Mkileta matawi hayo muyaweke getini kwa mlinzi.
  • Tarehe 05/03/2025 ni Jumatano ya MAJIVU. Kutakuwa na Misa tatu. Misa ya Kwanza itaanza saa 12:30 asubuhi, Misa ya Pili saa 7:00 mchana, na Misa ya Tatu itakuwa saa 10:30 jioni. Jumuiya za zamu zitahudumu katika Misa zote.
  • Viongozi wa Kanda mnaombwa kuwaandaa wazee na wahudumu kupakwa majivu katika Jumatano ya Majivu. Viongozi mnaombwa kuja kuwachukua wahudumu kuanzia saa 2:00 asubuhi karibu na Sakristia. Mnaombwa kuwaweka pamoja wazee na wagonjwa ili kurahisisha zoezi hilo.
  • Bahasha za Kwaresma zitagawiwa siku ya Jumatano ya Majivu. Kwa siku nyingine bahasha hizo zitakuwa zinapatikana pia kwenye stuli za masanduku pamoja na mlango mkubwa wa kuingia kanisani. Waamini mnaombwa kuzichukua na kuzirejesha kabla ya Pasaka.
  • Utoto Mtakatifu wa Yesu wanatarajia kufanya matendo ya huruma kipindi cha Kwaresma. Jumuiya zinaombwa kuwawezesha watoto kufanikisha lengo lao. Viongozi wa Jumuiya mnaombwa kuchukua barua elekezi getini.
  • Kutakuwa na ibada ya Njia ya Msalaba siku za Ijumaa katika kipindi cha Kwaresma. Ibada hiyo itaanza saa 06:00 mchana. Jioni pia kutakuwa na Njia ya Msalaba itakayoanza saa 11:00 ikifuatiwa na Misa Takatifu.
  • Tarehe 07/03/2025 siku ya Ijumaa, KANDA ya VATICAN na BETHLEHEMU, na Kwaya ya MT. GEMMA GALGAN, wataongoza Njia ya Msalaba na kutoa vipaji.KANDA YA YERUSALEMU na NAZARETH, na Kwaya ya MT. AUGUSTINO wajiandae.
  • Walezi wa utoto Mt. Pamoja na Makatekista mnatangaziwa kuwa kutakuwa na Semina elekezi kuhusu ulinzi wa mtoto hapa Parokiani. Semina itaanza tarehe 7 – 9/3/2025 kuanzia saa tisa alasiri katika ukumbi wa Inyasi. Walezi wote mnaombwa kushiriki bila kukosa.
  1. Waamini mnakumbushwa kutunza vitu vyenu kama simu, fedha, na pochi muwapo kanisani.
  1. Alhamisi tarehe 06/03/2025 Padre atawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Kanda ya SAMARIA. Alhamisi ijayo tarehe 13/03/2025 wajiandae Kanda ya YUDEA. Viongozi wa Kanda mnaombwa kumchukua Padre karibu na Ofisi ya Parokia saa tatu kamili asubuhi.
  1. Tunawashukuru Jumuiya ya MT. FRANCIS JEROME  na  B.M.T.L  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. RITA WA KASHIA na (B) MT. KAROLI LWANGA  Jumuiya ya MT. MARIA GORETH  na MT. ANDREA KAGWA wajiandae.
  1. NDOA.
  2. Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Gabriel Kitindi, wazazi wake ni Costantine Kitindi na Agnes Michael anataka kufunga ndoa na Neema Joab, wazazi wake ni Joab Thadayo na Maria Omary.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *