- Jumla kuu ya Fungu la kumi mwezi wa kumi na mbili (12) tumekusanya kiasi cha Tsh. 21,850,650/=
Paroko anawashukuru waumini wote waliotoa zaka ya mwezi wa kumi na mbili. Mungu awabariki nyote.
- Ofisi ya Parokia itafungwa kuanzia leo tarehe 05/01/2025 na kufunguliwa tarehe 14/01/2025.
- Jumomsi ijayo tarehe 11.01.2025 kutakuwa na misa ya upadrisho na ushemasi Jimboni itakayoanza saa nne kamili asubuhi. Waamini wote mnaalikwa kushiriki.
- Tunawashukuru wanajumuiya na wanaparokia wote kwa ujumla kwa majitoleo yenu ya sadaka na zaka ambayo yamefanya Parokia yetu kuwa washindi wa kwanza kidekania na kijimbo kwa mwaka 2024 kama ilivyotangazwa katika misa ya shukrani iliyofanyika katika Parokia ya Veyula jana. Ufafanuzi zaidi utatolewa Jumapili ijayo.
- Waamini waliofanya vipimo vya afya na kupewa dawa hapa Parokiani na Madaktari wa tiba mbadala(BF-Suma) wanaombwa kuwaona madaktari hao hapa Parokiani Jumapili ijayo tarehe 12.01.2025 kuanzia saa moja asubuhi hadi saa 12 jioni ili kujua maendeleo ya kiafya ya waamini hao. Pia watafanya vipimo kwa wale wanaohitaji huduma hiyo tarehe hiyo hiyo.
- Mafundisho ya ndoa kwa wanandoa watarajiwa yatakuwa tarehe 24-26/01/2024 hapa Parokiani.
- Tunawashukuru Jumuiya ya WAT. JOAKIM NA ANNA na MT. PAULO MIKI kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. YAHANE PAULO WA II na (B) MT. DOMINIKO. Jumuiya ya MT. ALOYCE GONZAGA na MT. JOSEPHINE BAKITHA wajiandae.
- NDOA.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Alisen Fredy, wazazi wake ni Renatus Majja na Carolina Flavia anataka kufunga ndoa na Victoria Leonard, wazazi wake ni Laurent Leonard na Jenista Mhagama.
MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:
Parokiayakiwanjachandege.or.tz.
NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish
KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:
YOUTUBE: Kndege Parish
FACEBOOK: Parokia Ya Kndege
INSTAGRAM: Kndege_Parish