Uncategorized

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 4 YA MAJILIO MWAKA ‘C’– 22/12/2024

  1. Leo tarehe 22/12/2024 Tamasha la Krismas Carols litaanza saa 10:00 jioni. Waamini wote mnakaribishwa kushiriki katika Tamasha hilo.
  • Kesho tarehe 23/12/2024 Misa ya Krismasi ya watoto itaanza saa 9:00 alasiri. Wazazi na walezi muwalete watoto mapema kwenye Misa yao bila kukosa.
  • Kesho tarehe 23/12/2024 kutakuwa na maungamo mara baada ya misa, kuanzia saa moja asubuhi hadi saa mbili kamili asubuhi; na Jumanne tarehe 24/12/2024 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana, na saa 9:00 alasiri hadi saa 11:00 jioni.
  • Jumanne tarehe 24/12/2024 Mkesha wa Krismasi utaanza saa 3:00 usiku. Watasimamia UWAKA na VIWAWA pamoja na kutoa vipaji.
  • Tarehe 25/12/2024 Misa zitakuwa kama kawaida, kama Jumapili. Watakaosimamia siku hiyo ya Krismasi ni WAWATA.
  • Tarehe 26/12/2024 kutakuwa na Misa mbili, ya kwanza itaanza saa 12:30 asubuhi, na misa ya ubatizo wa watoto itaanza saa 2:00 asubuhi. Watakaosimamia siku hiyo ni Moyo Mtakatifu wa Yesu na Shirika la Mt. Rita wa Kashia.
  • Tarehe 26/12/2024 kutakuwa na Ibada Maalumu ya Christimas ya Madhehebu mbalimbali huko Nyerere Square kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni. Nyote mnakaribishwa.
  • Tarehe 28/12/2024 kutakuwa na sherehe ya watoto mashahidi itakayofanyika Podium Mbwanga. Jumuiya zote mnaombwa kukamilisha mchango wa sherehe hiyo ambao ni sh. 100,000/= kwa kila jumuiya. Pia wazazi mnaombwa kuwanunulia watoto sare ya T-Sheti.
  • Jumamosi tarehe 28/12/2024 Wanaume wote wa Parokia ya K/Ndege watakuwa na Semina katika Kanda ya Samaria maeneo ya Shule ya Msingi Chinagali. Semina itaanza saa 9:30 Alasiri. Wanaume wote mnaombwa kuhudhuria.
  1. Watu wazima wasio na masakramenti mbalimbali mnaombwa kujiandikisha katika ofisi ya makatekista. Mafundisho yataanza Ijumaa tarehe 3/1/2025.
  1. Baba Paroko anaomba kukutana na madaktari na wauguzi wanaosali katika Parokia ya Kiwanja cha Ndege Jumapili ijayo tarehe 29.12.2024 mara baada ya misa ya pili katika ukumbi mdogo wa Parokia.  
  1. Chuo cha ufundi cha Don Bosco kilichoko Miyuji kinawatangazia nafasi za mafunzo ya ufundi stadi katika fani zote za ufundi kuanzia Januari 2025 kwa vijana wote waliomaliza Kidato cha Nne na Darasa la Saba. Kwa maelezo zaidi tazama tangazo katika ubao wa matangazo wa Parokia.  
  1. Tunashukuru Jumuiya ya MOYO MTAKATIFU WA YESU  na  MT. BIKIRA MARIA NYOTA YA ASUBUHI  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) WAT. JOACKIM NA ANNA na (B) MT. PAULO MIKI.  Jumuiya ya MT. DAVID LEWIS  na MT. FRANCIS BORGIA wajiandae.
  1. NDOA. (YASOMWE KATIKA MISA YA PILI TU)
  2. Kwa mara ya Tatu: Ndg. Godfrey Laurence, wazazi wake ni Laurence Yusuph na Regina Gombati anataka kufunga ndoa na Gloria Samwel, wazazi wake ni Samwel Elifamili na Saraphina Mabula.

MATANGAZO HAYA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA PAROKIA:

Parokiayakiwanjachandege.or.tz.

NA KWA APP YA PAROKIA: Kndege Parish                          

KWA VIDEO ZA MATUKIO YA PAROKIA TEMBELEA:

YOUTUBE: Kndege Parish

FACEBOOK: Parokia Ya Kndege

INSTAGRAM: Kndege_Parish

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *