- Mafundisho ya ndoa yatakuwa tarehe 20, 21 na 22/09/2024. Wanaotarajia kufunga ndoa wajiandikishe
- Watu wazima wasio na masakrament mbalimbali na wanatarajia kufunga ndoa wafike ofisi ya Parokia
kujiandikisha. - Tarehe 21/09/2024 tutakuwa na tamasha la Utoto Mtakatifu litakalofanyika hapa Parokiani kuanzia saa 8:00
Asubuhi hadi Saa 10:00 Jioni. Hivyo tunaomba wazazi na walezi wawaruhusu watoto kushiriki tamasha
hilo. - Tarehe 26/10/2024 kutakuwa na Hija ya watoto wote itakayofanyika kituo cha hija cha Sukamahela.
Tunawakumbusha viongozi, wazazi na walezi wa Jumuiya kuanza maandalizi mapema. Gharama ya hija ni
Tsh 18,500/= kwa kila mtoto. - Tarehe 18/09/24 siku ya Jumatano Padre atafanya ziara za kichungaji katika jumuiya ya MT. KAROLI
LWANGA na tarehe 20/09/24 siku ya Ijumaa katika Jumuiya ya MT. STEPHANO kuanzia saa 8:30
alasiri. Wiki ijayo wajiandae Jumuiya za MT. ANDREA KAGWA Na MT. NICHOLAUS OWEN. - Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye
Jumuiya zifuatazo MT. PHILIP EVANS, MT. STANSLAUS KOSTIKA, MT. FRANCIS JEROME,
MT. AGATHA, KRISTU MFALME, MT. JEAN MARIA MUZEEY. Jumapili Ijayo wajiandae
Jumuiya zifuatazo: MOYO MTAKATIFU WA YESU, B.M.T.L, MT. MAGRETH MARIA
ALACOQUE, MT. MARIA GORETI, MT. ALBERTO HURTADO, MT. BERNADETHA. Mama na baba
huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia. - Tunashukuru Jumuiya ya MT. STANSLAUS KOSTIKA na B.M.T.L kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia
utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. STEPHANO na (B) MT KAROLI LWANGA. Jumuiya ya
MT. RITA WA KASHIA, na MT. ANDREA KAGWA wajiandae. - NDOA. (YASOMWE KATIKA MISA YA PILI NA YA TATU TU)
a) Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Tadei Zenus, wazazi wake ni Zenus Kwangu na Lightness Zenus anataka kufunga
ndoa na Matrina John, wazazi wake ni Msafiri John na Jeni Amos.
b) Kwa mara ya Pili: Ndg. Costantine Marco, wazazi wake ni Marco Mwita na Mecktilda Melemo anataka
kufunga ndoa na Theresia Daniel, wazazi wake ni Daniel Patrick na Anna Onesmo.
c) Kwa mara ya Pili: Ndg. Denis Jairos, wazazi wake ni Jairos Samwel na Donatilda Emmanuel anataka kufunga
ndoa na Agnes Emily, wazazi wake ni Emily Mpululu na Dora Ernest.
d) Kwa mara ya Pili: Ndg. Imani Julias, wazazi wake ni Ernest Teendwa na Maria Ernest anataka kufunga ndoa
na Rita Mwima, wazazi wake ni Ambrose Mghanga na Rehema Akonaay.
e) Kwa mara ya Pili: Ndg. Astero Ntirihungwa, wazazi wake ni Laurence Ntirihungwa na Helena Singo anataka
kufunga ndoa na Rosemary Fortunatus, wazazi wake ni Fortunatus Lissu na Filbertha Lissu.
f) Kwa mara ya Tatu: Ndg. Aloyce Stephano, wazazi wake ni Stephano Mkonde na Ester Mkonde anataka
kufunga ndoa na Janeth Vecent, wazazi wake ni Vicent Madiyaga na Selina John.
g) Kwa mara ya Tatu: Ndg. Joseph Julius, wazazi wake ni Julius Machumbe na Ghati Machumbe anataka
kufunga ndoa na Stella Kichele, wazazi wake ni Kichele Mwita na Rose James.
2
Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.
Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH. app inapatikana playstore.
Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH
Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE
Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia
MATANGAZO YA DOMINICA YA 24 YA MWAKA ‘B’– 15/09/2024
14
Sep