MATANGAZO YA DOMINICA YA 23 YA MWAKA ‘B’– 08/09/2024
- Jumla kuu ya Fungu la kumi mwezi wa Nane tumekusanya kiasi cha Tsh. 20,546,100/=
Paroko anawashukuru waumini wote waliotoa zaka ya mwezi wa Nane. Mungu awabariki nyote.
- Kwaya ya Ledochowska inawashukuru waamini wote walioshiriki nasi katika kufanikisha mapokezi ya Wanakwaya kutoka Rwanda pamoja na Tamasha letu Mungu awabariki sana kwa majitoleo yenu.
- Tarehe 11/09/24 siku ya Jumatano Padre atafanya ziara za kichungaji katika jumuiya ya MT. JOSEPHINE BAKITA na tarehe 13/09/24 siku ya Ijumaa katika Jumuiya ya MT. AGATHA kuanzia saa 8:30 alasiri. Wiki ijayo wajiandae Jumuiya za MT. KAROLI LWANGA Na MT. STEPHANO.
- Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. CLARA WA ASISSI, MT. FRANCIS WA ASISSI, MT. ANDREA BOBOLA, WAT. JOACKIMU NA ANNA, MT. URSULA, MT. THERESIA WA MTOTO YESU.Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. PHILIP EVANS, MT. STANSLAUS KOSTIKA, MT. FRANCIS JEROME, MT. AGATHA, KRISTU MFALME, MT. JEAN MARIA MUZEEY.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
- Tunashukuru Jumuiya ya MT. ROBERT BELLARMIN na MT. KIZITO kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. FRANCIS JEROME na (B) MT ALBERTO HURTADO. Jumuiya ya MT. STEPHANO, na MT. KAROLI LWANGA wajiandae.
- NDOA. MATANGAZO HAYA YASOMWE KATIKA MISA YA PILI NA YA TATU TU
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Costantine Marco, wazazi wake ni Marco Mwita na Mecktilda Melemo anataka kufunga ndoa na Theresia Daniel, wazazi wake ni Daniel Patrick na Anna Onesmo.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Denis Jairos, wazazi wake ni Jairos Samwel na Donatilda Emmanuel anataka kufunga ndoa na Agnes Emily, wazazi wake ni Emily Mpululu na Dora Ernest.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Imani Julias, wazazi wake ni Ernest Teendwa na Maria Ernest anataka kufunga ndoa na Rita Mwima, wazazi wake ni Ambrose Mghanga na Rehema Akonaay.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Astero Ntirihungwa, wazazi wake ni Laurence Ntirihungwa na Helena Singo anataka kufunga ndoa na Rosemary Fortunatus, wazazi wake ni Fortunatus Lissu na Filbertha Lissu.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Aloyce Stephano, wazazi wake ni Stephano Mkonde na Ester Mkonde anataka kufunga ndoa na Janeth Vecent, wazazi wake ni Vicent Madiyaga na Selina John.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Joseph Julius, wazazi wake ni Julius Machumbe na Ghati Machumbe anataka kufunga ndoa na Stella Kichele, wazazi wake ni Kichele Mwita na Rose James.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Melkiori Majani, wazazi wake ni Severini Jumapili na Evangelista Khoaa anataka kufunga ndoa na Ester Bernard, wazazi wake ni Bernard Stephen na Anna Saulo.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Joseph Sefu, wazazi wake ni Ally Sefu na Christer Paulo anataka kufunga ndoa na Anastazia Richard, wazazi wake ni Richard Mankaba na Merana Augustino.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Dickson Sanga, wazazi wake ni Jimson Sanga na Bernadetha Nihume anataka kufunga ndoa na Magdalena Kibodya, wazazi wake ni Erasto Kibodya na Rehema Mgao.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Chrispo Nicholaus, wazazi wake ni Nicholaus Lwila na Betseba Lwila anataka kufunga ndoa na Dorothea Deodatus, wazazi wake ni Deodatus Mlokozi na Agnes Kokusimbisa.
Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.
Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH. app inapatikana playstore.
Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH
Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE
Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia