MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA 19 YA MWAKA ‘B’– 11/08/2024

  1. Jumapili tarehe 18/08/2024 kutakuwa na Semina ya Mavuno Misa zote. Uzinduzi wa mavuono mwaka huu utakuwa Jumapili ya tarehe 25/8/2023.
  • Waamini wanawake wenye changamoto ya kufika katika vyoo vilivyoko mwisho wa parking wanaombwa kutumia vyoo vilivyoko katika ukumbi wa Mt. Inyasi, karibu na vyoo vya walemavu. Vivyo hivyo, waamini wanaume wenye changamoto hiyo, wanaombwa kutumia vyoo vilivyoko karibu na konteina.  
  • Waumini mtakaorudisha bahasha za fungu la kumi wakati wa misa mnaombwa kuja mbele ya altare wakati wa kuleta shukrani ili mpate baraka maalum kabla ya kuzitumbukiza katika zanduku la bahasha.   
  • Kwaya ya Ledochowska inawatangazia waamini kuwa Tiketi za Tamasha lao zinapatikana hapo nje kwa gharama ya 10,000/= kwa watoto, 20,000/= kwa watu wazima na 100,000/= kwa VIP. Tamasha litafanyika tarehe 25/8/2024. Nyote mnakaribishwa.
  • Jumamosi Tarehe 17/08/2024 Misa ya Ubatizo wa watoto  itaanza saa 3:00 Asubuhi.
  • Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo B.M.T.L, MT. MAGRETH MARIA ALACOQUE, MT. MARIA GORETH, MT. ALBERTO HUTADO, MT. BERNADETHA, MT. YUDA THADEI. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. NICHOLAUS OWEN, MT. ANDREA KAGWA, MT. ALPHONSUS RODRIGUEZ, MT. KAROLI LWANGA, MT. ROBERT BELLARMINE, MT. ANTONY WA PADUA.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
  • Tunashukuru Jumuiya ya MT. YOHANE PAULO WA II  na  MT. JOSEPHINE BAKHITA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. PIO na (B) MT AGATHA.  Jumuiya ya MT. MAGRETH MARIA ALACOQUE,  na MT. SIMONI ZELOTE wajiandae.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Kedmon Mnyamagola, wazazi wake ni Leonard Mnyamagola na Magdalena Mnyamagola anataka kufunga ndoa na Rehema Wilson, wazazi wake ni Wilson Chilamba na Siflasi Mnyiri.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Yoshua Emmanuel, wazazi wake ni Emmanuel Youze na Merina Richard anataka kufunga ndoa na Merina David, wazazi wake ni Michael David na Narowil Sabaya.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Mathei Kalisti, wazazi wake ni Kalisti Mwibu na Petronila Zakaria anataka kufunga ndoa na Happyness Gasto, wazazi wake ni Gasto Tito na Leah Zabron.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Kelvin Ladislaus, wazazi wake ni Ladislaus Kilonda na Christina Ngajiro anataka kufunga ndoa na Mariam Gerson, wazazi wake ni Gerson Mangula na Sevelina Funguo.

Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.

Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH.  app inapatikana playstore.

Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH

Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *