MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA 18 YA MWAKA ‘B’– 04/08/2024

  1. Jumla kuu ya Fungu la kumi mwezi wa Saba tumekusanya kiasi cha Tsh. 23,033,500/=

Paroko anawashukuru waumini wote waliotoa zaka ya mwezi wa saba. Mungu awabariki nyote.

  • Wajumbe wa H/Walei mnatangaziwa kuwa Mkutano utakuwa Jumamosi tarehe 10/8/24. Viongozi wa Jumuiya na Vyama vya Kitume mnaombwa kuchukua barua getini. 
  • Kwaya ya Ledochowska inawatangazia waamini kuwa Tiketi za Tamasha lao zinapatikana hapo nje kwa gharama ya 10,000/= kwa watoto, 20,000/= kwa watu wazima na 100,000/= mzunguko wa wakubwa Tamasha litafanyika tarehe 25/8/2024. Nyote mnakaribishwa.
  • Tarehe 10/8/2024 kutakuwa na Semina ya Wazazi na Wasimamizi wa watoto watakao batizwa tarehe 17/8/2024. Semina itafanyika katika ukumbi wa Parokia kuanzia saa 3:00 asubuhi.
  • Jumuiya zitakazo adhimisha somo wao mwezi huu wa nane ni kama zifuatavyo:-  Mt. Dominico, Mt. Peter Febar, Mt. Clara wa Asissi, Mt. Maximilian Kolbe, Mt. Bikira Maria Nyota ya Asubuhi, Mt. Alberto Hurtado, Mt. Monica na Mt. Augustino. Viongozi mnaombwa kupitia ubao wa matangazo kuangalia tarehe za misa.
  • Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. FRANCIS JEROME, MT. AGATHA, MT. STANSLAUS KOSTIKA, KRISTU MFALME, MT. JEAN MARIA MUZEEY, MOYO MTAKATIFU WA YESU. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:B.M.T.L, MT. MAGRETH MARIA ALACOQUE, MT. MARIA GORETH, MT. ALBERTO HUTADO, MT. BERNADETHA, MT. YUDA THADEI.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
  • Tunashukuru Jumuiya ya MT. DAVID LEWIS  na  MT. DOMINICO  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. ALOYCE GONZAGA na (B) MT JOHN DE BRITO.  Jumuiya ya MT. PIO,  na MT. AGATHA wajiandae.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Kedmon Mnyamagola, wazazi wake ni Leonard Mnyamagola na Magdalena Mnyamagola anataka kufunga ndoa na Rehema Wilson, wazazi wake ni Wilson Chilamba na Siflasi Mnyiri.
  • Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Yoshua Emmanuel, wazazi wake ni Emmanuel Youze na Merina Richard anataka kufunga ndoa na Merina David, wazazi wake ni Michael David na Narowil Sabaya.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Mathei Kalisti, wazazi wake ni Kalisti Mwibu na Petronila Zakaria anataka kufunga ndoa na Happyness Gasto, wazazi wake ni Gasto Tito na Leah Zabron.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Kelvin Ladislaus, wazazi wake ni Ladislaus Kilonda na Christina Ngajiro anataka kufunga ndoa na Mariam Gerson, wazazi wake ni Gerson Mangula na Sevelina Funguo.
  • Kwa mara ya Tatu: Ndg. Albert Wagili, wazazi wake ni Joseph Sabeli na Josephina Ngiliule anataka kufunga ndoa na Rose Mbuva, wazazi wake ni Leons Safari na Everilda Buli.

Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.

Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH.  app inapatikana playstore.

Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH

Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE   

Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *