MATANGAZO YA DOMINICA YA 16 YA MWAKA ‘B’– 21/07/2024

- Wajumbe wa H/Walei mnatangaziwa kuwa Mkutano utakuwa tarehe 10/8/24. Viongozi wa Jumuiya na Vyama vya Kitume mnaombwa kuwasilisha ajenda. Mwisho wa kupokea ajenda ni tarehe 28/7/24.
- Kamati ya Hija Imeandaa safari ya Hija Kibeho Rwanda kuanzia tarehe 3/9/2024 hadi 10/9/2024. Safari hiyo itapitia Butiama kwa mtumishi wa Mungu Mwl. Julias Nyerere na Gharama ni 350,000/= wanaohita kwenda mnaombwa kujiandikisha Getini kwa Mlinzi.
- Tarehe 28/7/2024 waamini wote mnaombwa kuwashika mkono Makatekista na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kuwafundisha watoto wetu.
- Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. JOSEPHINE BAKITA, MT. YOHANE PAULO WA II, MT. MAXIMILIAN KOLBE, MT. YOHANE WA MSALABA, MT. CLARA WA ASISSI, MT. YUDA THADEI. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. GABRIEL MALAIKA MKUU, MT. ANDREA BOBOLA, WAT. JOACKIMU NA ANNA, MT. URSULA, MT. THERESIA WA MTOTO YESU, MT. PHILIPO EVANS.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
- Tunashukuru Jumuiya ya MT. PAULO MIKI na MT. MICHAEL MALAIKA MKUU kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. DAVID LEWIS na (B) MT DOMINICO. Jumuiya ya MT. YOHANE PAULO WA II, na MT. JOSEPHINE BAKITA wajiandae.
- Kwa mara ya Pili: Ndg. Andrew Julius, wazazi wake ni Julius Mselemu na Salvatorian Katunzi anataka kufunga ndoa na Mary Exaud, wazazi wake ni Axaud Mbise na Apaikunda Matayo.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. David John, wazazi wake ni John Mgawe na Santina Ignas anataka kufunga ndoa na Grace Raymond, wazazi wake ni Raymond Lucas na Veneranda Francis.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Frank Alex, wazazi wake ni Alex Amandus na Monica Petro anataka kufunga ndoa na Revinelight Focus, wazazi wake ni Focus Magwesela na Elizabeth Mashinanga.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Emmanuel Jaylos, wazazi wake ni Jaylos Jetulyo na Edith Benedicto anataka kufunga ndoa na Jojina Aulelian, wazazi wake ni Aulelian Benedict na Levina Petro.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Edson James, wazazi wake ni James Yohana na Consolata Damian anataka kufunga ndoa na Asha Ally, wazazi wake ni Ally Mbwambo na Halima Abdala.
_________________________________________________________________________________________________
Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.
Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH. app inapatikana playstore.
Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH
Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE
Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia