MATANGAZO

MATANGAZO YA DOMINICA YA 15 YA MWAKA ‘B’– 14/07/2024

  1. Wajumbe wa H/Walei mnatangaziwa kuwa Mkutano ambao ulikuwa ufanyike tarehe 20/7/24 umeahirishwa hadi tarehe 10/8/24. Viongozi wa Jumuiya na Vyama vya Kitume mnaombwa kuwasilisha ajenda.  Mwisho wa kupokea ajenda hizo ni tarehe 28/7/24.
  • Tarehe 29/7/2024 waamini wote mnaombwa kuwashika mkono Makatekista na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kuwafundisha watoto wetu.
  • Mafundisho ya ndoa yatakuwa tarehe 19, 20 na 21/07/2024. Wanaotarajia kufunga ndoa wajiandikishe.
  • Makatekista wanaendelea kuandikisha watoto wa mafundisho ya Kipaimara, Komnyo ya Kwanza na watu wazima wa masakiramenti mbalimbali. Mwisho wa kuandikisha ni tarehe 30/7/2024.
  • Kamati ya Hija Imeandaa safari ya Hija Kibeho Rwanda kuanzia tarehe 3/9/2024 hadi 10/9/2024. Safari hiyo itapitia Butiama kwa mtumishi wa Mungu Mwl. Julias Nyerere na Gharama ni 350,000/=
  • Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. PETER CLAVERY, MT. AUGUSTINO, MT. GEMMA GALGAN, MT. MONICA, MT. ANTONY DANIEL, MT. DAVID LEWIS. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. JOSEPHINE BAKITA, MT. YOHANE PAULO WA II, MT. MAXIMILIAN KOLBE, MT. YOHANE WA MSALABA, MT. CLARA WA ASISSI, MT. YUDA THADEI.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
  • Tunashukuru Jumuiya ya MT. PETER FEBAR   na  MT. JOSEPHINE BAKITA  kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) WAT. JOACKIMU NA ANNA na (B) MT FRANCIS BORGIA.  Jumuiya ya DAVID LEWIS,  na MT. DOMINICO wajiandae.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. David John, wazazi wake ni John Mgawe na Santina Ignas anataka kufunga ndoa na Grace Raymond, wazazi wake ni Raymond Lucas na Veneranda Francis.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Frank Alex, wazazi wake ni Alex Amandus na Monica Petro anataka kufunga ndoa na Revinelight Focus, wazazi wake ni Focus Magwesela na Elizabeth Mashinanga.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Emmanuel Jaylos, wazazi wake ni Jaylos Jetulyo na Edith Benedicto anataka kufunga ndoa na Jojina Aulelian, wazazi wake ni Aulelian Benedict na Levina Petro.
  • Kwa mara ya Pili: Ndg. Edson James, wazazi wake ni James Yohana na Consolata Damian anataka kufunga ndoa na Asha Ally, wazazi wake ni Ally Mbwambo na Halima Abdala.

Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.

Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH.  app inapatikana playstore.

Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH

Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE   

Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *