
- Jumla kuu ya Fungu la kumi mwezi wa Sita tumekusanya kiasi cha Tsh. 24,711,500/=
Paroko anawashukuru waumini wote waliotoa zaka ya mwezi wa sita. Mungu awabariki nyote.
- Jumapili tarehe 14/7/24 kutakuwa na uapisho wa Viongozi wa Jumuiya waliochaguliwa kuziba nafasi mbalimbali za viongozi na chaguzi ndogo zilizofanyika. Uapisho huo utafanyika katika Misa ya pili.Viongozi mfike bila kukosa.
- Jumapili tarehe 14/7/24 kutakuwa na Misa tatu tu. Misa ya I saa 12:00 asubuhi, Misa ya II saa 1:00 asubuhi na Misa ya Tatu itakuwa ya Kipaimara ni saa 4:00 asubuhi. Hakuta kuwa na Misa ya watoto.
- Wazazi na walezi mnaombwa kuchukua fomu za Ubatizo wa watoto wachanga. Ubatizo utakaotakuwa tarehe 17/8/2024.
- Ratiba ya Misa mwezi wa Saba inapatikana katika ubao wa matangazo.
- Makatekista wanaendelea kuandikisha watoto wa mafundisho ya Kipaimara, Komnyo ya Kwanza na watu wazima wa masakiramenti mbalimbali. Mwisho wa kuandikisha ni tarehe 30/7/2024.
- Kamati ya Hija Imeandaa safari ya Hija Kibeho Rwanda kuanzia tarehe 3/9/2024 hadi 10/9/2024. Safari hiyo itapitia Butiama kwa mtumishi wa Mungu Mwl. Julias Nyerere na Gharama ni 350,000/=
- Leo mara baada ya Misa ya pili, Masista watawapelekea wagonjwa na wazee Ekaristi Takatifu kwenye Jumuiya zifuatazo MT. ALPHONCE RODRIGUEZ, MT. KAROLI LWANGA, MT. ROBERT BELLARMINE, MT. ANTONY WA PADUA, MT. PAULO MIKI, MT. FRANCIS BORGIA. Jumapili Ijayo wajiandae Jumuiya zifuatazo:MT. PETER CLAVERY, MT. AUGUSTINO, MT. GEMMA GALGAN, MT. MONICA, MT. ANTONY DANIEL, MT. DAVID LEWIS.Mama na baba huruma mnaombwa kuwachukua Masista karibu na Sakristia.
- Tunashukuru Jumuiya ya MT. THERESIA WA MTOTO YESU na MT. FRANCIS WA ASISSI kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Juma lijalo ni zamu ya (A) MT. PAULO MIKI na (B) MT. MICHAEL MALAIKA MKUU. Jumuiya ya WAT. JOCKIMU NA ANNA, na MT. FRANCIS BORGIA wajiandae.
- NDOA.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Frank Alex, wazazi wake ni Alex Amandus na Monica Petro anataka kufunga ndoa na Revinelight Focus, wazazi wake ni Focus Magwesela na Elizabeth Mashinanga.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Emmanuel Jaylos, wazazi wake ni Jaylos Jetulyo na Edith Benedicto anataka kufunga ndoa na Jojina Aulelian, wazazi wake ni Aulelian Benedict na Levina Petro.
- Kwa mara ya Kwanza: Ndg. Edson James, wazazi wake ni James Yohana na Consolata Damian anataka kufunga ndoa na Asha Ally, wazazi wake ni Ally Mbwambo na Halima Abdala.
- Kwa mara ya Tatu: Ndg. Mwita Vincent, wazazi wake ni Samson Chacha na Veronica Daniel anataka kufunga ndoa na Sarah Matika, wazazi wake ni Daniel Mwendi na Lois Julius.
Matangazo haya yanapatikana katika tovuti ya parokia:PAROKIAYAKIWANJACHANDEGE.OR.TZ.
Pia yanapatikana kwa App ya parokia: KNDEGE PARISH. app inapatikana playstore.
Kwa video ya matukio ya parokia tembelea youtube chanel: KNDEGE PARISH
Facebook ya parokia ni: PAROKIA YA KNDEGE
Waumini mnaombwa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbalimbali za parokia